Meneja masoko wa SEMES Atupele Elias akionyesha moja ya mashine za kufanyia usafi katika ofisi mbalimbali na numba mjini Arusha.
Baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya SEMES wakiwa katika picha ya pamoja.
NA GLADNESS MUSHI WA FULLSHANGWE-ARUSHA
KAMPUNI ya Semes ya jijini la Arusha imeweka mikakati ya kuhakikisha kuwa inawaakomboa wanamke wa nchi ya Tanzania kwa kuwapa elimu ya ujasiriamali sanjari na kuwapatia mitaji ili iwawezeshe kujikwamua kiuchumi.
Hayo yalisemwa na mkurugenzi wa kampuni hiyo Bw Elias Seme alipokuwa katika sherehe za kuzindua kikundi cha kampuni hiyo jijini hapa
Alisema kuwa ili kuhakikisha kuwa wanawake wanaondokana na hali ya utegemezi kampuni hiyo imejipanga kuhakikisha kuwa wanawake wanapewa kipaumbele katika kuwakomboa kwa kuwapatia mitaji mbali mbali .
Alieleza kuwa mwanamke ndie mwenye huruma na ana uwezo wa kupangilia mipango zaidi ya wanaume hivyo wanayo fursa kubwa ya kuwezeshwa ili waweze kujikwamua kiuchumi
Bw Seme aliongeza kuwa kampuni hiyo tayari.imeshatoa mitaji ya shilingi milioni tano kwa mwaka huu ambapo pia wameweza kuanzisha vikoba kwa lengo la kukopeshana ili kuboresha maisha yao
Aliongeza kuwa mbali na hayo kampuni hiyo imefanikiwa kutoa ajira kwa vijana 21 ambapo lengo halisi ni kuweza kutoa ajira kwa watu 50-60 kwa mwaka .
Akielezea changamoto inayoikabili kampuni hiyo alisema kuwa ni pamoja na ushindani wa kibiashara ambapo kumekuwepo na makampuni mengi kutoka nchi ya nje yanayohusiana na maswala ya usafi hivyo kuwepo na upinzani mkubwa.
Alitaja mikakati waliyonayo kuwa ni pamoja na kuongeza vitega uchumi zaidi na kujiboresha ili iweze kujiongezea mapato zaidi ili kuwawezesha vijana wengi kujipatia ajira.
No comments:
Post a Comment