Tuesday, May 8, 2012

UINGEREZA: WAZEE WA HEAVY DAVID HAYE NA DERECK CHISORA KUPAMBANA TAREHE 14 JULAI MWAKA HUU.


Brawlers: Dereck Chisora (left) and David Haye went head to head in Munich
                                                                     
 Chisora na Haye 
 David Haye na Dereck Chisora wanatazamiwa kupanda ulingoni na kupambana tarehe 14 Julai, katika pambano lililoidhinishwa na shirikisho la ngumi la Luxemboug.
Meneja wa Chisora Frank Warren, amesema pambano hilo litafanyika katika mtaa wa Upton Park, Uingereza.
Mabondia hao wawili wa uzani wa heavy waligombana na kuanza kumenyana katika mkutano wa waandishi wa habari, mara tu baada ya Chisora kutandikwa mjini Munich na bondia Vitali Klitschko mwezi Februari.Head-to-head: Haye has vowed to knock out Chisora when they finally clash inside the ring
Bodi ya mchezo wa ngumi nchini Uingereza ilikataa kuidhinisha pambano hilo, kwani mabondia wote wawili hawana leseni ya Uingereza inayowaruhusu kupambana.
Uamuzi kufuatia rufaa ya Dereck Chisora kutetea uamuzi wa kumpokonya leseni umecheleweshwa, na Frank Warren amekasirishwa sana na namna bodi ya Uingereza ya ngumi ilivyoshughulikia suala hilo
.Hammer time: Haye sits with trainer and manager Adam Booth during the press conference at West Ham's football ground
“Kwa wengi ni vigumu kuvumilia kuwaona Chisora na David Haye hatimaye wakinufaika kutokana na tukio la fedheha mjini Munich, lakini katika ngumi, tukio kama hilo ni chanzo cha pambano la kusisimua zaidi litakaloweza kufanyika katika nchi hii”.
Chisora alipokonywa leseni kufuatia matukio kadha kabla na baada ya pambano lake dhidi ya Klitschko.

Kati ya matukio hayo, Chisora, mwenye umri wa miaka 28, alimpiga kofi Klitschko kutoka Ukraine, wakati mabondia hao wawili walipokuwa wakipimwa uzani, na kisha kumtemea maji ndugu yake, Wladimir, kabla ya pambano hilo.Match maker: Promoter Frank Warren sits beside Chisora
Kwa upande wake, Haye aliisalimisha leseni yake mwezi Oktoba mwaka jana, miezi mitatu baada ya kushindwa na Wladimir mjini Hamburg, Ujerumani, katika pambano la kuwania mkanda wa WBA.Caged beats: Ring rivals Haye and Chisora are put at bay by a steel fence to ensure there is no repeat of their shameful brawl in Munich
Awali Warren alikuwa amesema hana nia ya kusimamia pambano kati ya Chisora na Haye.

Lakini amesema amebadilisha nia,

Tale of the tape: Chisora v Haye
kwa kuona rufaa ya Chisora kutaka leseni sasa imesukumwa hadi mwezi Julai.
Warren anakiri kwamba alilofanya Chisora ni jambo la kipumbavu, na anastahili adhabu.


Lakini anasema bondia huyo atakuwa nje ya ulingo miezi sita, na ana haki ya kujipatia pesa na riziki yake maishani.

No comments: