Saturday, May 26, 2012

LAKE ZONE YAZIDI KUTOA MAFUNZO KWA MADEREVA KAGERA

Kamanda wa polisi mkoa wa Kagera Bw. Henry Salewi akikabidhi vyeti kwa wahitimu kati ya wahitimu hao wapo viongozi wa serikali wakiwemo watendaji wa kata na polisi.

Kamanda wa polisi mkoa wa Kagera Bw. Henry Salewi akizungumza wakati wa hafla fupi ya kufunga mafunzo ya muda mfupi kwa madereva wa magari na pikipiki yaliyofanyika kata ya Kyebitembe wilayani Muleba, ambapo yaliwashirikisha zaidi ya madereva 76.




Mkurugenzi wa chuo cha mafunzo ya udereva mkoa wa Kagera cha lake zone Bw. Winston Kabantega, akiwa na Wp Rose, chuo cha lake zone kilichopo mjini Bukoba kinaelezwa na kamanda wa polisi mkoa wa Kagera Bw. Salewi kuwa msaada mkubwa kwa jeshi la polisi katika kuelimisha madereva na hatimaye kupunguza ajali za mara kwa mara kulinganisha na miaka kaadha iliyopita.
Mkurugenzi wa chuo cha mafunzo ya udereva mkoa wa Kagera cha lake zone ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya usalama barabarani mkoa Bw. Winston Kabantega,akitoa maelezo juu mafunzo ya muda mfupi kwa madereva yaliyoandaliwa na chup hicho kwa kushirikiana na jeshi la polisi kikosi cha usalama barabarani mkoa wa Kagera, lengo likiwa ni kuwarahisishia madereva waliopo vijijini kupata leseni ili kupunguza ajali.



Ni baadhi ya wahitimu wa mafunzo hayo wakila kiapo mbele ya mgeni rasmi kamanda wa polisi mkoa wa Kagera Henry Salewi wakihaidi kufuata sheria za usalama barabarani walizofundishwa ili mkupunguza ajali wilayani huo, ambapo wilaya hiyo inadaiwa kuongoza kwa ajali za barabarani tofauti na wilaya nyingine za mkoani hapa.
Sehemu ya wahitimu wa mafunzo wakifuatilia hotuba mbalimbali zilizokuwa, ambapo pamoja na  mambo mingine  wametakiwa  kufuata sheria za barabarani na kujihami wanapoendesha vypmbo vya moto.


Wahitimu hawa wanasoma risala kwa mgeni rasmi huku wakieleza a mambo yaliyofundishwa ambayo baadhi yake ni pamoja na polisi jamii, alama za barabarani, ukaguzi wa vyombo vya moto na uzimaji wa moto.

No comments: