Meneja wa United, Alex Ferguson. Wanahitaji miujiza kutetea unigwa wao
Manchester United wameendelea kuweka ndoto zao za kutetea ubingwa wao kwa kuichapa Swansea kwa mabao 2-0.
United walijitahidi kutaka kufunga mabao mengi ili kupunguza tofauti iliyopo kati yao na Manchester City, lakini walipoteza nafasi nyingi za kufanikisha hilo. Ashley Young akitupia nyavuni kufanya goli ziwe mbili katika kipindi cha kwanza.
Manchester City wanaendelea kuongoza ligi wakiwa pointi sawa na United, lakini wana magoli 8 zaidi.
Manchester City watatangazwa kuwa mabingwa wiki ijayo iwapo wataichapa QPR, hata kama Manchester United watashinda mchezo wao wa mwisho dhidi ya Sunderland.
Sir Alex Ferguson (kushoto) na Wayne Rooney kwa machungu wakifukuzia ubingwa ligi kuu England
Iwapo United watataka kuchukua ubingwa, watalazimika kupata ushindi wa magoli zaidi ya manane huku wakizingatia matokeo yatakayopatikana kati ya City na QPR.
Iwapo United watataka kuchukua ubingwa, watalazimika kupata ushindi wa magoli zaidi ya manane huku wakizingatia matokeo yatakayopatikana kati ya City na QPR.
No comments:
Post a Comment