Thursday, November 29, 2012

MAPYA YAIBUKA TRENI YA DK MWAKYEMBE DAR

 Baadhi ya Wakazi wa Jiji la Dar wakiwa wanasubiri treni ya mwakyembe iwasili stesheni ikitokea ubungo maziwa tayari kwa safari ya kuwarudisha Majumbani Kwao. Baadhi ya Abiria wakiwa wamewahi kwaajili ya Kupanga foleni ili waweze kupata siti huku wengine wakichuchumaa kutokana na kulisubiri kwa muda
 Abiria Wakiteremka katika treni linalofanya safari zake ndani ya Jiji la Dar mara lilipowasili Katika Kituo cha Stesheni karibu na central polisi tayari kwa safari ya kurudi tena Ubungo
Baadhi ya Abiria waliogeuza na treni hilo wakiwa wamepandia Kituo cha Kamata Ili kuwahi Siti ambapo walipelekea sintofahamu kwa baadhi ya abiria waliokuwa kituoni hapo na kutaka kupanda kwenye hilo behewa kukuta likiwa tayari limeshajaa kutoka na abiria kugeuza na treni hilo wakati utaratibu huwa haurusiwi na ikifika mwisho abiria wote wanatakiwa kushuka
 
Abiria wakianza kupanda treni tayari kwa kurejea makwao mara baada ya treni la mwakyembe kuwasili kituoni hapo kwenye majira ya saa kumi na moja na dakika ishirini jana
 Mmoja wa Abiria aliyegeuza na treni hilo ambapo walipandia Kamata kwa lengo la kuwahi kiti akibishana na mmoja katika ya abiria ambao walikua kwenye foleni muda mrefu wakisubiria treni hilo kufika ili waweze kuingia ndani na kupata siti ambapo alikuta behewa hilo likiwa limeshajaa na kuanza kubishana huku abiria waliokuwa wakisubiri treni hilo wakitaka abiria waliogeuza na treni hilo kushuka
Wakazi wa Jiji la Dar wakiwa kwenye foleni ya kupanda treni maarufu kwa jina la treni ya mwakyembe jana kwenye majira ya saa 11 jioni katika kituo cha Stesheni tayari kwa kurudi nalo ubungo huku baadhi ya behewa kuwa limeshajaa kabla hata halijafika kituoni hapo kutokana na abiria kugeuza nalo kwa lengo la kuwahi siti. Behewa ambalo lilikuja likiwa limeshajaa ni behewa lenye namba 3644 ambalo abiria wake walikua wamepandia njiani kwa nia ya kugeuza nalo ili waweze kupata siti.
Wakazi wa jiji la Dar wakipanda kwenye treni la mwakyembe mara baada ya kuwasili kwenye kituo chake cha Stesheni jana Kwenye majira ya Saa 11 Jioni jana tayari kwa kuwarudisha majumbani kwao likitokea Mjini kuelekea Ubungo ambapo ndio kituo cha Mwisho
Na Josephat Lukaza – Lukaza Blog
 
Katika hali isiyo ya kawaida jana kwenye majira ya Saa 11: 20 Jioni katika kituo cha Treni kilichopo stesheni mkabala na Kituo Cha Polisi Cha Cetral kuliibuka Jambo la kushangaza wakati abiria wanaosubiria treni inayofanya kazi zake ndani ya jiji la dar kuona behewa moja likiwa limeshajaha tayari kutokana na abiria kupandia njiani na kugeuza nalo kwa lengo la kuwahi siti na kupelekea abiria waliowahi kituoni hapo na  kupanga foleni kwaajili ya kuwahi siti kuambulia patupu.
 
Abiria waliokuwa wakisubiria treni hilo walianza kulalamika pale ambapo walikuta behewa hilo limeshajaa kabla hata treni hiyo haijafika kwenye kituo chake cha mwisho kwa lengo la abiria hao kuwahi .
 
 Baada ya Tukio hilo kutokea kulizuka sintofahamu kwa baadhi ya wafanyakazi na Askari Polisi ambao hawajawahi kuona utaratibu huo ukifanyika na kupelekea Abiria kuhisi tayari wafanyakazi wa treni hiyo waneshaanza kuchakua kitu ambacho utaratibu hauruhusu.
 
 Utaratibu uliopo ni kwamba hata kama abiria amepandia katikati anatakiwa kuteremka pindi treni hilo linapofika mwisho wa kituo ndipo akate tiketi kwaajili ya kupanda tena na kurudi nalo lakini hali imekuwa tofauti hapo jana baada ya abiria hao kutokushuka na tiketi kukatiwa ndani na kupelekea abiria waliokuwa wakisubiri treni hilo kusubiri kwa muda mrefu.
Lukaza blog imeweza kunakili sauti za abiria ambao waliokuwa wakilalamika juu ya utaratibu huo uliofanywa na wafanyakazi ambao sio waaminifu na kupelekea usumbufu kwa abiria ambao wamewahi kupanga foleni.

No comments: