Ndugu zangu, tumesoma tamko la pamoja la wanaharakati wa Jukwaa La Katiba ( Bara) na Baraza la Katiba Zanzibar , angalia; http://www.mjengwablog.com/ 2012/05/wanaharakati-wakemea- vitisho-katiba.html#comment- form
Tamko lile linanikumbusha mjadala niliouanzisha Disemba mwaka jana kwa kuutolea kisa cha Mtema Kuni. Soma nilichoandika wakati huo na mjadala uliofuatia;
"Ndugu zangu,
Kwenye hili la mchakato wa kupata katiba mpya bado nasimama kwenye kauli yangu ya tangu mwezi Aprili mwaka huu, kuwa tumeanza na mguu mbaya lakini naamini kuwa bado tuna nafasi ya kujisahihisha.
Ndio, tukitanguliza hekima na busara tunaweza kuinusuru nchi yetu tuliyozaliwa kwa madhara ya muda mrefu yatakayotokana na makosa tunayotaka kuyafanya kwa makusudi kwa kutanguliza zaidi maslahi ya kisiasa ya muda mfupi.
Matukio ya hivi karibuni
Niwe mkweli kwa nchi yangu, katika hili la mchakato wa katiba naanza kuziona dalili za uwepo wa mizengwe ya kisiasa inayouzunguka mchakato wenyewe.
Ni mizengwe inayozingua akili za Watanzania kuliko kuzituliza. Na katika dunia ya sasa, nchi itakayounda katiba yake itakayotokana na mizengwe ya kisiasa badala ya hoja za msingi za kitaifa, kamwe haiwezi kuwa na hakika ya kubaki salama.
Tayari, kwenye muswada uliokwishatiwa saini na Mheshimiwa Rais Jakaya Kikwete, kuna vifungu vya.... Soma zaidi: http://www.kwanzajamii.com
No comments:
Post a Comment