Godbless Lema akiwasili Same
Katibu Mkuu wa TLP Same, Heriel Msolo(kulia) akirudisha kadi jana
CHADEMA wanaziara ya kichama Wilayani Same kwa siku nne, kuanzia jana hadi jumatatu chini ya Mwenyekiti wa Baraza la Vijana BAVICHA, Ngd Jhon Heche.
Wana mikutano maeneo tofauti ya Wilaya katika kuimarisha chama hicho.
Mkutano wa jana ulifanyikia viwanja vya Kwasakwasa Mjini Same kuanzia saa 9 hadi saa 12 jioni
Viongozi waliohudhuria ni pamoja na aliekuwa mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema, Mwenyekiti Bavicha, John Heche, Mweyekiti CHADEMA Kilimanjaro, Augustino Matemu na kiongozi wa vijana Babati, Wilson Mattaka.
Wengine ni James Ole Millya aliekuwa Mwenyekiti UVCCM Arusha, aliekuwa Mjumbe wa NEC CCM kutoka Arusha, Ndg Ally Bananga na aliekuwa Diwani wa Sombetion (CCM). WOte hawa walihamia CHADEMA mapema mwezi huu
Katika mkutano huo kadi nyingi sana zilitolewa na kuasiniwa na John Heche..tena zikigombewa kununua. Lema litoa ofa ya kadi 10 kwa kina mama na Millya nae akatoa ofa ya kuwalipia vijana kumi..
Aliekuwa Katibu Mkuu wa TLP Same, Ndg Heriel Msolo alirudisha kadi ya TLP na kupewa kadi ya CHADEMA na Mwenyekiti wa BAVICHA, John Heche
Lema aliwataka watanzania kutokubali kugwanywa na wanasiasa kwa misingi ya udini na ukabila au ukanda na kueleza kwamba CHADEMA haipiganii maslahi ya kundi lolote katika hayo. Akasema hata yeye hapiganiimaslahi yake binafsi bali ya watanzania.
John Heche aliwataka watanzania kujitokeza kutoa maoni yao kwa tume ya Katiba na kuelekeza kuwa wakatae au wazifanyie mabadiliko makubwa nafasi za uDC au uRC na nyinginezo za kuteuliwa na mtu mmoja. Akadai pia madaraka ya rais ni makubwa na mamabo mengi yameachwa kwa mtu mmoja. hali inayohitaji marekebisho ili kuwe na uwajibikaji wa pamoja..
Na Seria Tuma
No comments:
Post a Comment