Saturday, May 12, 2012

DA!!!! FILIKUNJOMBE

Mapokezi Ya Filikunjombe Yatikisa Ludewa

Mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe akiwa katika usafiri wa punda baada ya kupokelewa leo jimboni kwake kutokana na uamuzi wake wa kutia sahihi katika fomu maalum bungeni ya kutokuwa na imani na waziri mkuu Mizengo Pinda na kupelekea kuvunjwa kwa baraza la mawaziri hivi karibuni
kiongozi wa Chadema wilaya ya Ludewa akiwa katika mkutano wa kumpokea mbunge Deo Filikunjombe sasa ,mkutano unaoendelea uwanja wa mpira wa Ludewa mjini
Wakazi wa Ludewa wakiwa na mabango yenye jumbe mbali mbali za kumpongeza mbunge wao Deo Filikunjombe kwa kupambana na ufisadi
Maandamano makubwa ya kumpokea mbunge wa Ludewa Deo Filikunjombe (CCM)
Mbunge wa jimbo la Ludewa akiwa katika usafiri wa punda baada ya kupokelewa na kutembea zaidi ya kilometa 5 hadi mjini Ludewa leo
Baadhi ya wanafunzi wanaosomesha na mbunge Filikunjombe Ludewa waki
Vyama vya upinzani na CCM Ludewa vyaungana katika mapokezi hayo
Maandamano makubwa ya kumpokea shujaa wa kupambana na vitendo vya ufisadi mbunge Deo Filikunjombe leo

No comments: