Monday, May 7, 2012

MKUU WA MKOA KAGERA AONESHA JIPAJI CHAKE KWA KULA SEBENE

Haya ndio mambo ya maadhimisho ya uhuru wa vyombo vya habari yaliyoandaliwa na chama cha waandishi wa habari Kagera (KPC), hapa anaonekana mkuu wa mkoa wa Kagera Kanali Mstaafu Fabian Massawe akisakata rumb.Alionesha kipaji hicho akiwa anacheza kwa hisia na kutulia kwani pale ambapo mzikiulioweka ulipomkosha.Ni jambo la kujivunia kwa akazi wa mkoa wa Kagera kwani wana kiongozi mwenye kuonesha kupenda burudani.

Mwandishi wa habari mkongwe Bw Nsherenguzi akisakata rumba na kamanda wa Taasisi ya kupambana na kuzuia rushwa (TAKUKURU) wa mkoa wa Kagera Bi Domina Mkama.

Mkuu wa mkoa wa kagera Kanali Mstaafu Fabian Massawe akiwahutubia waandishi wa habari walipofanya sherehe ya maadhimisho ya uhuru wa vyombo vya habari kwenye ukumbi wa hoteli ya coffee iliyoko kwenye manispaa ya Bukoba, alikuwa akiwaasa waachane na tabia ya kuandika taarifa zenye lengo la kuleta uvinjifu wa amani ndani ya jamii.



Katibu wa chama cha mapinduzi (CCM) wa mkoa wa Kagera akiwaasa waandishi wa habari wazingatie miiko ya taaluma yao.Chini yake na Mwandishi mkongwe Mr.Method Kalikila akiwa na Jonas

Baadhi ya waandishi walioudhuria sherehe hizo, wanaoneka wakiburudika kwa vinywaji vya aina mbalimbali.katikati ni Mr.Antidius Kalunde,Daniel Limbe akifuatiwa na mwanadada Ashura Jumapili kushoto ni Juhudi Felix akifuatiwa na Theonestina Juma
Mkuu wa mkoa wa Kagera akiweka jiwe la msingi kwenye jengo la chama cha ushirika mkoani Kagera (KCU 1990) lililopo karibu na standi kuu ya mabasi ya mji wa Bukoba.

No comments: