Monday, May 7, 2012

NAENDA MTAA WA PILI NITAKUWA NAKUJA KUWAONA SAWA??????????????

Ndugu zangu, 
Ukitaka  kumjua Mwafrika, basi, mwangalie siku anapohama. Ndivyo tulivyo. Hata kwenye uongozi, ni hivyo hivyo. Mwangalie kiongozi wa Afrika anapoingia
na anapotoka kwenye madaraka.

Ndio, hana tofauti sana na Mswahili anayehama kutoka Mwananyamala kwenda Magomeni. Mswahili wa
Mwananyamala, hata kama atahakikishiswa, kuwa anakohamia Magomeni vyumba
vyote vina taa za balbu na pazia za madirishani na milangoni, bado,
Mswahili huyu atahakikisha, kabla ya kuhama, anang’oa balbu na pazia
zote kutoka nyumba anayohama. Mpangaji mpya atakayekuja atajua mwenyewe!
Huyo ndio Mwafrika, ingawa si wote, hata ukimchanja kwenye damu yake,
utakuta chembe chembe za ushamba uliochanganyika na hila.

Hakika, hizo ni hulka za Mwafrika, hata azaliwe na kukulia Ulaya au Marekani.

No comments: