Afisa Elimu Mkoa Iringa Ndg. Joseph Mnyikambi akimkabidhi zawadi mshindi wa mbio za baiskeli walemavu km.5 Kasim Kasilo wa Iringa aliyeibuka mshindi wa kwanza. Amejipatia jumla ya pesa Tsh. 50.000/=
Mary Naali toka Arusha akipokea zawadi ya Ushindi wa kwanza km. 21 wanawake katika mbio za Ruaha Marathon toka kwa Afisa Elimu Mkoa Iringa Ndg. Joseph Mnyikambi.
.Alphonce Ferix toka Arusha akipokea zawadi ya ushindi wa kwanza kwa wanaume km. 21 toka kwa mgeni rasmi Ndg. Joseph Mnyikambi Afisa Elimu Mkoa Iringa kwenye mashindano ya Ruaha Marathon Iringa.
Alphonce Ferix mshindi wa kwanza km. 21 wanaume, alitumia muda wa saa 1:03:9 akipongezwa na Dada Nansi Mawele
Mery Naary akipongezwa baada ya kumaliza mbio kwa muda wa saa 1:13:01 kwa wanawake km. 21
Kasim Kasilo akipongezwa baada ya kuibuka kidedea katika mbioza baiskeli walemavu Ruaha marathon Iringa umbali wa kilomita 6.
No comments:
Post a Comment