Monday, May 7, 2012

SONGOMA AWEKA WAZI KILA KITU

Na Sifael Paul
MGANGA wa tiba asilia a.k.a Sangoma aliyejizolea umaarufu mkubwa jijini Dar es Salaam, Salum Jongo amekiri kuwa katika kipindi alichopokea waheshimiwa wengi ni wakati Rais Jakaya Kikwete alipopewa baraka na Halmashauri Kuu (CC) ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kuunda baraza jipya la mawaziri.
Jongo aliliambia The Biggest IQ Paper, Ijumaa Wikienda mwishoni mwa wiki iliyopita kuwa katika kipindi hicho alikuwa akipokea simu nyingi kutoka kwa baadhi ya mawaziri wakitaka dawa ili wasipoteze nyadhifa zao na wabunge waliokuwa wakihitaji kuingia kwenye baraza jipya.
“Nimepokea tenda nyingi kutoka kwa mawaziri na wabunge waliotaka niwafanyie mambo waingie kwenye baraza jipya na kweli wapo waliofanikiwa (majina yapo),” alisema Jongo na kuongeza:
“Kuna wengine hawakuja direct (moja kwa moja), lakini waliwatuma ndugu zao kwa sababu walihofia kuonekana.”
MAWAZIRI WALIOPENYA
Katika baraza jipya la mawaziri, waliopenya ni Stephen Wasira, George Mkuchika, Celina Kombani, Samia Suluhu, Dk. Terezya Huvisa, Mary Nagu, Hawa Ghasia na William Lukuvi.
Wengine ni Samuel Sitta, Shamsi Vuai Nahodha, Dk. John Magufuli, Dk. Hussein Mwinyi, Dk. Shukuru Kawambwa, Sophia Simba, Bernard Membe, Mathias Chikawe, Dk. Emmanuel Nchimbi, Dk. David Mathayo na Gaudencia Kabaka.
Waliofunga listi ni Prof. Makame Mbarawa, Prof. Anna Tibaijuka, Prof. Jumanne Maghembe, Prof. Mark Mwandosya, Injinia Christopher Chiza, Dk. Harrison Mwakyembe, Dk. Fenella Mukangara, Khamis Kagasheki, Abdallah Kigoda, Dk. William Mgimwa na Prof. Sospeter Muhongo.


No comments: