Monday, May 7, 2012

MAMA LULU CHUPU CHUPU

Mama mzazi wa Elizabeth Michael ‘Lulu,’ Lucresia Karugila.
Elizabeth Michael ‘Lulu,’.
Shakoor Jongo na Musa Mateja
MAMA mzazi wa supastaa wa sinema za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu,’ Lucresia Karugila anadaiwa kuikimbia nyumba anayoishi kwa kile kilichoelezwa ni kuwakwepa mashabiki wa marehemu Steven Charles Kanumba ‘The Great’ ambao wamekuwa wakivamia na kumtishia kifo baada ya mwanaye kuhusishwa na kifo cha staa huyo kipenzi cha watu.
Kwa mujibu wa chanzo makini, mama Lulu ameikimbia nyumba hiyo iliyopo Tabata Kimanga jijini Dar es Salaam tangu Aprili 20, mwaka huu ambapo kwa sasa anaishi Mwananyamala Komakoma kwa rafiki kipenzi wa Lulu aliyetajwa kwa jina moja la Muna.
KAULI YA JIRANI MMOJA
“Jamani hivi mna habari kwamba mama Lulu siku hizi anaishi Mwananyamala Komakoma kwa rafiki yake Lulu aitwaye Muna? Nasikia huyo Muna ni ndugu na msanii wa maigizo mmoja mwenye jina kubwa.
“Huku Tabata ni kuchungu, tangu mwanaye akamatwe kwa kifo cha Kanumba, mashabiki wa marehemu wamekuwa wakienda kwake na kumtishia kifo.
“Lakini pia ndugu wa mama Lulu na marafiki, nao wamechangia huyu mama kukimbia nyumba kwa sababu kila kukicha walikuwa wakijaa tele eti kumpa pole, mama wa watu akaona cha kufia nini, akatimua,” kilisema chanzo hicho.

MALEZI MABAYA YA LULU NAYO YATAJWA
Chanzo chetu kikazidi kudai kwamba mbali na mashabiki wa Kanumba kumtishia kifo mwanamke huyo, pia walikuwa wakimkejeli kwamba malezi mabaya ndiyo kiini cha mwanaye kumfika makubwa.
“Halafu hao mashabiki bwana, wakawa wanamwambia mama wa watu kuwa malezi mabaya ya mwanaye ndiyo yamemfanya afikwe na mazito kama yaliyomfika,” kilidai chanzo.

SAUTI YA MAMA LULU
Baada ya kunyetishiwa nyeti hizo, The Biggest IQ Paper, Ijumaa Wikienda lilimwendea hewani mama huyo ili kutaka kujua juu ya madai hayo.
Mwandishi: Haloo … natumaini naongea na mama mzazi wa Lulu eeh?
Mama Lulu: Ndiyo baba, wewe nani mwenzangu?
Mwandishi: Naitwa Musa Mateja wa Global Publishers.
Mama Lulu: Unasemaje mwanangu?

Mwandishi: Mama tuna taarifa kuwa umekimbia nyumbani kwako..?
Mama Lulu: Haaa... unasemaje?
Mwandishi: Taarifa zimetufikia kwamba umekimbia nyumbani kwako Tabata kutokana na mashabiki wa marehemu Kanumba kuja kila wakati wakikutishia maisha na kukujeli?
Mama Lulu: Jamani jamani… naombeni mambo ya kesi ya Lulu tuiachie mahakama.
Mwandishi: Mama mimi sijakupigia simu kuzungumzia keshi ya mwanao, nataka uniambie kama kweli umetimka nyumbani kwa madai hayo?

Mama Lulu: Sasa mimi nikiondoka kwangu nyinyi inawahusu nini?
Mwandishi: Hapa ninapozungumza na wewe tupo nyumbani kwako Tabata lakini hatujakuta mtu na majirani ndiyo wamesema haupo.
Mama Lulu: Mimi mbona nyumbani nimeondoka nikamuacha mama yangu mzazi labda kama yeye ndiyo kawaambia maneno hayo mseme!
Mwandishi: Mama nakwambia tumeambiwa na majirani na mama yako sisi hatujamkuta hapa.
Mama Lulu: Sikia mwanangu habari hizo sizitaki maana nimechoka kufuatwafuatwa, hata kama sipo kwangu au sipo, sitaki habari hizo.

Mwandishi: Mama mbona hujanijibu sasa swali langu la msingi?
Mama Lulu: Mimi nipo kwangu na sikai Mwananyamala naomba nieleweke hivyo jamani… maana mambo ya hiyo kesi yako mahakamani na kama mnataka kujua zaidi muulizeni Lulu mwenyewe, mimi sitaki kuandikwa gazetini!

Mwandishi: Oke, asante mama Lulu.
Mama Lulu: Haya mwanangu.
MUNA NAYE
Naye Muna anayesemekena kumhifadhi mama Lulu alipopatikana kwa simu yake ya mkononi na kuulizwa kuhusu madai hayo alisema ana mambo mengi ya kufanya huku akikata simu.



No comments: