Thursday, May 10, 2012

TUJENGE BUKOBA YETU


Barabra hii iko mtaa wa Kashenye imekatika na hivyo kusababisha usumbufu kwa watumiaji barabara hiyo, uko mtaa wa Kashenye uliko katika kata ya kashai, mtaa wa Kashenye ni moja ya mitaa iliyoko katika manispaa ya Bukoba ambayo imesahaulika mtaa huu ni moja ya mitaa yenye miundo mbinu hatarishi.
Muonekano wa barabara inayounga mtaa wa Kashenye na maeneo mengine ya Manispaa ya Bukoba, hapa ni mtaa wa maduka sita, barabara hii haipitiki ni imewasababisha baadhi ya wakazi kuhamia mitaa mingine.
Haya ni madhari ya barabara iliyoko eneo la kilimanjaro lililopo kata ya Kashai inayounga mtaa wa Kashenye na maeneo mengine yaliyoko mkoani Kagera.
 
Uongozi wa halmashauri ya manispa ya Bukoba unawachanganya wananchi, hii inatokana na hatua yake ya kutaka kutekeleza miradi mikubwa ya mabilioni na kusahau miradi yenye ustawi mkubwa kwa jamii, wananchi wanataka manispaa kabla ya kutekeleza miradi mikubwa kwanza itekeleze miradi midogo ambayo ni pamoja na kuzifanyia ukarabati barabara, hii inatokana na hatua ya manispaa ya kuitelekeza miundo mbinu barabara iliyoko mtaa wa Kashenye jambo ambalo limeufanya mtaa huo uonekane kama kisiwa ndani ya manispaa ya Bukoba.
Manispaa hiyo kwa sasa inaipa kipaumbele miradi mikubwa inayotaka kuitekeleza ambayo ni pamoja na ujenzi wa soko kuu, standi kuu ya mabasi na jengo la kibiashara ambayo itagharimu mabilioni ya pesa, wananchi wanadai kuwa manispaa kutekeleza miradi hii kabla ya kuleta ustawi miongoni mwao itakuwa inawatelekeza wananchi wa mtaa wa Kashenye kwa kuwa barabara zote hazipitiki na hivyo itakuwa inaendelea kuwatenga na wananchi waishio maeneo mengine
yaliyoko ndani ya manispaa.

No comments: