Friday, May 11, 2012

ROY HODGSON KUTANGAZA KIKOSI CHA ENGLAND CHA UERO 2012 MEI 16

PATAKUWA HAPATOSHI

Meneja mpya wa England, Roy Hodgson, akizungumza na vyombo vya habari amesemq kuwa  atatangaza Kikosi chake Jumatano Mei 16 kwa ajili ya Mashindano ya Mataifa ya Ulaya, EURO 2012, yatakayochezwa huko Nchini Poland na Ukraine.
Hodgson atakuwa huru kubadili Kikosi hicho hadi Siku ya mwisho Mei 29 ambapo UEFA ndio wanataka Nchi zote zitakazocheza EURO 2012 ziwe zimewasilisha Vikosi vyao kwao.
Timu ya England inatarajiwa kujumuika hapo Mei 21 na kwenda kwenye Kambi ya mazoezi ya Siku 4 huko Spain.
Kabla ya EURO 2012, England itacheza Mechi za kirafiki mbili na Norway hapo Mei 26 huko Oslo na kisha kucheza Uwanjani Wembley na Belgium hapo Juni 2.
Mechi ya kwanza ya England huko EURO 2012, ambao wako Kundi D, ni dhidi ya France Juni 11 Mjini Donestk, Ukraine.

KUNDI D
Ukraine
Sweden
France
England

MECHI ZAKE - Kuchezwa Nchini Ukraine:
Juni 11: France v England [Mjini Donetsk Saa 1 Usiku]
Juni 11: Ukraine v Sweden [Kiev Saa 3 Dak 45 Usiku]
Juni 15: Sweden v England [Kiev Saa 1 Usiku]
Juni 15: Ukraine v France [Donetsk Saa 3 Dak 45 Usiku]
Juni 19: Sweden v France [Kiev Saa 3 Dak 45 Usiku]
Juni 19: England v Ukraine [Donetsk Saa 3 Dak 45 Usiku]

No comments: