Thursday, June 14, 2012

BABA KANUMBA HASHANGAZA WATU

BABA: HAKUNA HAJA YA KUKARABATI KABURI LA KANUMBA



Na Gladness Mallya
BABA mzazi wa marehemu Steven Kanumba, Charles Kusekwa (pichani) amefunguka kuwa hajui kama kuna haja ya kulijenga kaburi la mwanaye tena kwa kuwa wasanii wenzake walishalikarabati.
Kauli hiyo imekuja baada ya hivi karibuni mama Kanumba, Flora Mtegoa kutaka baba huyo aulizwe kuhusu suala la kujenga kaburi hilo ili liwe katika hali ya kuridhisha badala ya kukaa na kushindania mali alizoziacha Kanumba.
Baada ya kusikiliza maneno ya mama huyo, paparazi wetu alimtafuta baba Kanumba kwa njia ya simu ambapo alifunguka:
“Haa! Kaburi la Kanumba si limeshakarabatiwa na wasanii wenzake, haina haja ya kulijenga tena labda baadaye baada ya kumaliza mambo ya mirathi kwani kwa sasa ndiyo suala muhimu zaidi.”

No comments: