Monday, June 18, 2012

NAPE AMPASHA MBUNGE MSIGWA AMTAKA KUJIANDAA KUACHIA JIMBO 2015

Na Blog ya  Francis Godwin

katibu wa itikadi na uenezi wa Chama cha mapinduzi ( CCM) Taifa Bw. Nape Nauye amekiri kuwa CCM ilipoteza jimbo la Iringa mjini kwa makosa yake na kuwa kosa hilo kamwe halitarudiwa tena na kumfananisha mbunge wa jimbo hilo Mchungaji Peter Msigwa kuwa ni msindikizaji wa CCM katika jimbo hilo.

Kwani alisema kuwa kosa lililofanyika katika uchaguzi mkuu mwaka 2010 kwa kushindwa kuongoza kura za ubunge ni kutokana na makosa yaliyojitokeza hivyo kupelekea madiwani kushinda na Rais Jakaya Kikwete kupata ushindi mkubwa ila ubunge baada ya yule waliomchagua wana CCM Frederick Mwakalebela jimbo hilo lilichukuliwa na upinzani kosa ambalo kamwe halitarudiwa tena.

Asema vyama vya upinzani ni vyama vya wanaharakati kwa ajili ya kuikumbusha serikali ya CCM kwa pale inapokosea na sio kuja kuongoza nchi.

Pia Nauye aliuagiza uongozi wa serikali ya mkoa wa Iringa kuhakikisha unafungua mara moja barabara ya Magereza inayoelekea Hospitali ya mkoa ambayo imekuwa ikichangia usumbufu wa wagonjwa Kwenda kutibiwa.

Akiwahutubia wakazi wa jimbo la Iringa mjini katika viwanja vya Soko kuu Leo ,Nauye alisema kuwa moja Kati ya kilio kikubwa kwa wakazi wa mji wa Iringa ni hatua ya uongozi wa Magereza Iringa kuifunga barabara hiyo kwa ajili ya matumizi ya Magereza mkoa wa Iringa jambo ambalo linasababisha usumbufu kwa wananchi wanaofika Hospitali hiyo ya mkoa.

Hivyo alisema tayari amemwagiza mkuu wa mkoa wa Iringa DKT Christina Ishengoma kuhakikisha anasimamia zoezi hilo ili barabara hiyo ifunguliwe na kupunguza kero za wananchi na wagonjwa wanaofika kutibiwa katika Hospitali hiyo ya mkoa.

No comments: