Wednesday, June 13, 2012

VIJANA WATAKIWA KUJIONGEZA KATIKA MAMBO YA MSINGI

Vijana watakiwa kufanya utafiti

Afisa wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (ACTECH) Bwana Saleh Mikidadi akitoa maelezo mbele ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar balozi Seif Ali Iddi aliyefungua rasmi Ofisi ya Tume hiyo pamoja na ile ya Nguvu za Atomiki iliyopo katika Jengo la Ofisi ya Makamu wa Rais wa Jmauhuri ya Muungano liliopo Tunguu, nyuma ya Afisa Mikidadi ni Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia wa Serikali ya Muungano, Makame Mnyaa Mbarawa
Uongozi wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia Tanzania {costech} umeombwa kushajiisha Wasomi hasa Vijana wa Vyuo Vikuu Nchini kupenda kufanya tafiti mbali mbali zitakazojenga Mazingira ya kumuondoa Mtanzania kwenye matatizo yanayomkabili. 

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ametoa ombi hilo katika Hafla fupi ya uzinduzi wa Ofisi ya Tume hiyo ilyofanyika hapo Tunguu Mkoa wa Kusini Unguja. Balozi Seif alisema Tafiti kama hizo ambazo zitakuwa na uhusiano wa moja kwa moja na Mwananchi zinaweza kusaidia kupata Maendeleo kwa kasi zaidi katika Kipindi kifupi kijacho.
Alisisitiza kwamba Serikali kwa upande wake iko tayari kwa namna yoyote ile kutumia vyema matokeo ya Tafiti zinazofanywa na Wazomi wazalendo.
Hata hivyo Balozi Seif alieleza kuwa yapo baadhi ya matokeo ya Tafiti hubakia kuwa siri kwa Taifa lakini mengine yanastahiki kutolewa kwa Wananchi ili waelewe kinachoendelea kwenye maisha yao.
Balozi Seif alieleza kwamba wakati umefika kwa Makampuni pamoja na Viwanda vya hapa Nchini kujenga Utamaduni wa kutoa kazi zao za Utafiti kwa Tume hiyo ili ijipatie fedha za kuendesha shughuli zake za utafiti kama Nchi nyengine zilizoendelea.
Alieleza kwamba Tanzania imepania kuleta maendeleo kwa Wananchi wake kutokana na uamuzi wake wa kutenga Jumla ya shilingi za Kitanzania Bilioni Thalathini { 30,000,000,000/-} kwa ajili ya Utafiti na Maendeleo kwenye Bajeti yake ya Mwaka 2010/2012.
Balozi Seif alifahamisha kwamba Maendeleo bila ya Sayansi na Teknolojia hayapatikani kwani masuala hayo mawili yanakaribiana katika utekelezaji wake.
Akizungumzia Tume ya Taifa ya nguvu za Atomu Balozi Seif alielezea kufarajika kwake kutokana na mipango m,izuri ya Taasisi hiyo kuhudumia Zanzibar katika masuala ya usimamizi wa matumizi salama ya Mionzi. Balozi Seif alisema ushirikiano wa pamoja wa Taasisi hiyo,Wizara ya Afya Zanzibar na Shirika la Nguvu za Atomiki Duniani katika kuanzisha mradi wa Matibabu ya Saratani katika Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja unafaa kuungwa mkono.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ameishukuru Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa uamuzi wake wa wa kusogeza karibu na Wananchi shughuli za Ofisi ya Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia na Ofisi ya Tume ya Taifa ya Nguvu za Atomu.
Katika Taarifa yake Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania Profesa Iddi Suleiman Nyangarika Mkilaha alisema Taasisi yake itaendelea kutoa Elimu sahihi ya matumizi ya Mionzi. Profesa Nyangarika alisema Taaluma hizo kwa sasa itazingatia zaidi katika sekta ya Viwanda pamoja na Vituo vya Afya ambavyo vinatumia Vifaa vyenye mazingira ya Nguvu za Atomiki.
Mkurugenzi huyo wa Tume ya Nguvu za Atomiki alifahamisha kwamba katika kupanua zaidi huduma zake Taasisi hiyo itaendelea kupima Mionzi katika Mimea ili kujua kiwango sahihi cha kulinda Vyakula kwa ajili yamatumizi bora kwa Wanaadamu. Mapema Waziri wa Mawasiliano,Sayansina Teknolojia wa Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Makame Mnyaa Mbarawa alisema Wizara hiyo itaendelea kushirikiana na Wataalamu wa ndani na nje ili kuona Tafiti zinazofanywa zinatmika kwa walengwa ambao ni Wananchi.
Alisema Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia na ile ya Nguvu za Atomiki zimeanzishwa zikiwa na wajibu wa kusimamia tafiti na nguvu za Atomiki Nchini kwa kushirikiana na Taasisi za Kanda na zile za Kimataifa.

No comments: