Wednesday, July 18, 2012

Hatimaye Serikali Ya Uingereza Yakubali Kesi Ya Wapigania Uhuru Ma Kenya "Mau Mau"




Serikali ya Uingereza inasema ni kweli wanajeshi wake waliokuwa nchini Kenya kipindi cha ukoloni miaka ya hamsini na sitini waliwatesa na kukiuka haki za wapiganaji wa uhuru  waliofahamika kama Mau Mau.

Wazee watatu wanawaakilishi mamia ya wapiganiaji wa uhuru nchini Kenya ambao bado hai katika kesi wanayoishtaki serikali ya Uingereza kwa mateso waliyoyapata kipindi wakitaka kujitawala.

Mawakili wa wazee hao wamesema kuwa serikali ya Uingereza imetambua kesi hiyo,licha ya kusema kuwa miaka nyingi imepita kwa haki kupatikana kwa wapiganiaji hao wa Uhuru .

Aidha, mawakili wa wazee hao wanasema wana ushahidi wa kutosha wa faili elfu nane unaonyesha namna wakoloni walivyowatesa wakenya hao kabla ya taifa hilo kupata uhuru wake mwaka 1963.

Askofu wa zamani wa Afrika Kusini Desmond Tutu amemwandikia barua Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron kuishutumu serikali yake kwa kukiuka haki za msingi za wazee hao.

Kesi ya wapiganiaji Uhuru hao inaendelea ambapo wanataka kufidiwa na serikali ya Uingereza kwa mateso waliyoyapata. Wakenya hao waliwasilisha kesi hiyo kwa mara ya kwanza  mwaka 2009.

No comments: