Wednesday, July 25, 2012

Mafunzo 1st EAC-GIZ Masterclass Photography yaendelea Arusha



 NAIBU Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), anayeshughulikia Shirikisho la Kisiasa, Dkt. Julius Rotich (kushoto) akifungua mafunzo ya siku tatu ya upigaji picha yajulikanayo kama ‘EAC-GIZ Master Class Photographers Training’ yaliyoanza Julai 23-26, 2012 mjini Arusha. Kulia ni Mkuu Mawasiliano na Mahusiano wa EAC, Owora Richard Othieno.
  Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), anayeshughulikia Shirikisho la Kisiasa, Dkt. Julius Rotich(akifafanua jambo kwa waandishi juu ya Mafunzo ya Upigaji picha ‘EAC-GIZ Master Class Photographers Training’
 Mkufunzi Mkuu wa Upigaji picha ambaye pia ni Mpigapicha kutoka Ujerumani ambaye anafanya shughuli zake nchini Kenya, Hartmut Fiebig akitoa maelekezo kwa wapigapicha.
 Bruno Birakwate (kushoto) na Jennifer Muiruri wakisikiliza kwa makini mafunzo hayo
 Wapigapicha wakiwa darasani wakifuatilia mafunzo
 Mkufunzi Mkuu wa Upigaji picha ambaye pia ni Mpigapicha kutoka Ujerumani ambaye anafanya shughuli zake nchini Kenya, Hartmut Fiebig akitoa maelekezo kwa wapigapicha.
Mpigapicha Mroki Mroki kutoka Tanzania, akihojiwa na vyombo vya habari kuhusiana na mafunzo hayo ya Upigajipicha.
 Washiriki wa warsha ya wapiga picha kutoka nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wakiwa katika picha ya pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa EAC anayeshughulikia Shirikisho la Kisiasa Dr Julius Rotich (aliyeketi wa pili kushoto) mjini Arusha jana. Kushoto kwake ni Kaimu mkuu wa mpango wa EAC-GIZ and kulia ni Mkuu wa Idara ya Habari EAC Owora Othieno. Kulia kabisa aliyesimama ni mratibu wa mafunzo wa EAC Sukhdev Chhatbar

No comments: