Thursday, July 19, 2012

Matukio Ya Uokoaji Ajali Ya Meli Zanzibar


 
Waziri wa Biashara Viwanda na Masoko Nassor Mazrui, akitoka katika eneo la tukio jana usiku. 
Vijana wa Red Cross wakiwa katika bandari ya Malindu wakisubiri majeruhi na maiti wa ajali ya boti ya abiria.
Boti ya Kampuni ya Azam Marine ikiwasili katika bandari ya Malindi ikiwa na baadhi ya abiria waliookolewa
 Madakatari wa Hospitali Kuu ya Taifa ya Mnazi Mmoja wakitowa huduma kwa majeruhi waliofikishwa hospitalini hapo kwa uchunguzi zaida.
Majeruhi  wa ajali ya Boti kutoka nje ya Nchi ambao ni watalii waliokuwa wakija Zanzibar kutembea kwa ajili ya Utalii wakiwasili katika hospital kuu ya Mnazi Mmoja kwa kupata huduma zaidi wakisaidiwa na wahudumu wa huspitali hiyo 
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif  Ali Iddi, akizungumza na Daktari bingwa wa kufanya uchunguzi wa maiti wa ajali kupitia uchunguzi wa kuchukua vinasaba DNA, Dk. Ahmed Makata,  Makamu alipotembelea eneo maalum la kuwekea miili ya maiti wa ajali ya Boti katika viwanja maisara.
Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Abdalla Mwinyi Khamis akiwa na Mkuu wa Jeshi la Polisa Tanzania Said Mwema alipofika viwanja vya maisara kuangalia shughuli za utambuzi wa maiti zinavyoendelea jana usiku.



Waokoaji wakiwa kazini kwenye Meli ya Kilimanjaro



Muokoaji akiwa na maiti


Waokoaji wakiwa na majeruhi kwenye moja ya Boti za uokoaji.


Majeruhi wa wakipatiwa matibabu kwenye Hospitali ya Mnazi Mmoja


MV KMKM ikiwa kazini


Raia wa kigeni wakiwasili Bandarini baada ya kuokolewa


Majeruhi wakipatiwa matibabu katika Hospitali ya Mnazi Mmoja






Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA) imesema, meli iliyozama jana katika kisiwa cha Chumbe, Zanzibar ilikuwa na abiria 248 wakiwemo watoto 31. 

Kwa mujibu wa Sumatra, meli hiyo, inamilikiwa na Kampuni Seagul Transport, imasajiliwa na Mamlaka ya Usafiri Baharini Zanzibar (ZMA) na kwamba, Cheti cha Ubora kimeanza tarehe 24 Agosti, 2011 na kinamalizika 23 Agosti, 2012. Imesema, meli hiyo ilikuwa imeruhusiwa kubeba abiria wanaoruhusiwa 300 na tani 26 za mizigo.

SUMATRA kupitia Kituo cha Utafutaji na Uokoaji (MRCC) ilipata taarifa kuwa meli ya MV Skagit iliyokuwa safarini kutoka Dar es Salaam kuelekea Zanzibar ilikuwa inazama katika eneo la karibu na kisiwa cha Chumbe, Zanzibar, eneo ambalo lipo umbali wa Kilomita za Bahari 13.8 kutoka Bandari ya Zanzibar.

Zoezi la uokoaji linaendelea katika eneo la tukio kutoka kwa Mv Flying Horse, Mv Kilimanjaro III, Tug Bandari ya Zanzibar, KMKM, Mv Zanzibar I, Police Patrol Boat, Navy.
Taarifa hizi ni kwa mujibu wa vyanzo mbali mbali.

No comments: