Sunday, July 29, 2012

Tamko La Vijana Dhidi Ya Kanisa La KKKT Dayosisi Ya Iringa.



Kanisa la kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) usharika wa kanisa kuu

A: UTANGULIZI

”BWANA yuko mbali na waovu, bali husikia maombi ya wenye haki” (Mith 15:29)

1. Awali ya yote kama vijana wa Kanisa Kuu tumefikishwa mahali ambapo lazima tuseme na kutenda. Tumechoshwa kabisa na chokochoko zisizoisha. Tumechoshwa kuona matusi yasiyotamkika kwenye mitaa, mabango, mitaro na kwenye vituo vya makusanyiko ya watu dhidi ya Askofu wetu. Mambo hayo mabaya yamefikia hatua ya kutufungia lango la Kanisa sisi tusiohusika, eti kwa kisingizio cha kumfungia Askofu ambaye hakuwepo kanisani wala hata ndani ya mji.

2. Sisi tunapenda kumshukuru Mungu kwa kutupa uhai na kutuimarisha zaidi na zaidi katika kumtumikia Mungu kupitia vipawa mbalimbali tulivyojaliwa na Mungu. Pamoja na tofauti ya vipawa hivyo mbalimbali, sote kwa pamoja kama Wakristo tunashirikiana vyema katika kueneza Injili na kuujenga mwili wa Kristo, kwa maana ndilo kusudi la Mungu katika wito wetu.

3. Kwa kuzingatia misingi ya Neno la Mungu (Ezekiel 3:17-58), Mungu anamtaka...... Soma zaidi: http://www.kwanzajamii.com

No comments: