Na Mashaka Baltazar wa Fullshangwe-MWANZA
*Kura 28 zamng'oa ,wanane wataka abaki
AlLIYEKUWA Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza,Bw.Josephat Manyerere ameng’olewa katika nafasi hiyo jana baada ya kupigiwa kura ya kutokuwa na imani naye na Madiwani,wakimtuhumu kutumia wadhifa wake vibaya,kushiriki vitendo vya rushwa na kushindwa kufanya kazi.
Tuhuma zingine dhidi ya Diwani huyo wa Kata ya Nyakato (CHADEMA) ni mwenendo mbaya wa ukosefu wa adabu ulemavu wa kimwili au kiakili kiasi cha kumfanya ashindwe kutekeleza majkumu yake kama mwenyekiti wa vikao vya halmashauri ya jiji.
Kutokana na kadhia hiyo, Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza Bw.Wilson Kabwe, aliwasilisha hoja ya Madiwani waliojiorodhesha na kufikia theluthi mbili ya wajumbe wapatao 17 kati ya wajumbe 33 wa vikao halali vya baraza la madiwani wa Jiji hilo,alidai suala hilo ni la kisheria na kanuni ya 80 za kudumu za halmashauri hiyo.
“Halmashauri inaweza kumuondoa Mwenyekiti au Meya madarakani kwa azimio linaloungwa mkono na theluthi mbili ya wajumbe kutokana na sababu yoyote ya ni (a) Kutumia nafasi yake vibaya(b),Kushiriki vitendo vya rushwa(c),Kushindwa kazi(d),Mwenendo mbaya wa ukosefu wa adabu na(e) ulemavu wa kimwili aidha kiakili kwa kiasi cha kumfanya kushindwa kutekeleza majukumu yake kama Mwenyekiti ama Meya.” Alifanunua Kabwe.
Tuhuma hizo kumi zilizowasilishwa kwa wajumbe na kusababisha kung’olewa kwake zilitajwa kwanza ni pamoja na kusimamia ujenzi wa kanisa moja bila kufuata utaratibu na kanuni za Halmashauri,kutoa maelezo kwa barua ya kushinikiza madiwani wenzake kuihoji na kupinga bajeti ambayo kimsingi na kikanuni bajeti hiyo niya kwakwe pia na ndiye msimamizi akiwa Meya.
Kabla ya kung’olewa akifungua kikao hicho aliyekuwa Meya Bw.Manyerere, baada ya kusomwa dua na baadhi ya madiwani kama alivyoomba Meya huyo kutokana na imani za dini za Kikristo na Kiislamu, ambapo Meya huyo alimwomba Katibu wa baraza hilo kusoma Ajenda ya kikao hicho cha dharula kwa wajumbe, kufuatia ombi la madiwani kwa barua yao waliyoiwasilisha tangu Mei 24 mwaka huu.
Kabwe ,alisema kuwa katika kikao hicho ajenda ni moja tu ya wajumbe kutokuwa na imani na Meya hivyo kanuni ya 80 ya kumuondoa madarakani waliyoomba itekelezwe lakini kabla ya kufanya uamuzi huo baraza hilo lilitakiwa kujibadili na kukaa kama kamati.
Meya Manyerere aliwahoji wajumbe 28 kati ya 33 waliohudhuria kikao hicho kulingana na kanuni,sheria na taratibu za halmashauri wanaokubali waseme hoja hiyo imeafikiwa na wanaopinga waseme hapana.
“Wajumbe hoja hiyo iliyotolewa, wanaosema ndiyo waseme inaafikiwa ambapo bila kujali itikadi zao za vyama vya siasa kwa kauli moja madiwani hao waliitikia Ndiyooooooooo!!! ”na hakuna madiwani waliopinga hoja hiyo kwa kusema hapana.
Baada ya kukubalika kwa hoja hiyo Mkurugenzi huyo wa Jiji,aliwataka watu wasio wajumbe wa kikao hicho cha Kamati kutoka nje ya ukumbi huku viongozi waalikwa waliongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhandisi Evarist Ndikilo,Katibu Tawala, Dorothy Mwanyika na Wakuu wa wilaya na Ilemela, Baraka Konisaga (Nyamagana) na Amina Masenza (Ilemela) wakitakiwa kubaki kwa mujibu wa taratibu za Halmashauri.
Baada ya hatua hiyo baraza lilirejea kama kawaida,ambapo lilisikiliza utetezi wa Meya Bw.Manyerere ambapo katika madai hayo kumi yaliyowasilishwa kuhusu tuhuma zilizokuwa zinamkabili kusomwa, alijitetea kabla ya kufanyika uamuzi wa wajumbe kupiga kura za kumuondoa madarakani ama kumuacha aendelee na nafasi yake ya Umeya.
Baada ya Naibu Meya kutangaza matokeo ya kura za kumng’oa Meya Manyerere aliwaambia Madiwani hao kwa kutumia kauli kama ilivyokuwa kwa aliyekuwa Waziri Mkuu katika utawala wa serikali ya awamu ya nne Bw.Edward Lowassa, alipojiuzulu wadhifa wake kufuatia sakata la kampuni ya kufua umeme ya Richmond,”.
“Tunapokezana kijiti,mimi siwezi kusikitika lakini kama ni kwa mtindo huo, hata aingie nani,hata aingie nani.Niwatakie eh shughuli njema kwa kuwa bado tunayo halmashauri yetu,baada ya kugawanywa kusema eti lakini provided bado tupo pamoja na basi sitaji feel sana inferior, kwa sababu ndiyo uamuzi wenu ndiyo mliniona;”
“Lakini niwaombe tu kwamba unapomchukia mtu kwa kitu,kwa sababu kuna ile chuki binafsi na kama hiyo ndiyo ita to read kwenye maongozi basi hatutafika.Basi nibaki tu kusema kama mheshimwa Lowassa alivyosema,kwamba kama shida ni Uwaziri Mkuu ? Basi kama shida ilikuwa ni Umeya basi is okay, nawatakia kazi njema na amani kwa bwana Sharom,”alisema Meya huyo wa zamani wa jiji la Mwanza,Manyerere
Naibu Meya wa Jiji hilo na Diwani wa Kata ya Mahina, Bw.Charles Chichibela (CHADEMA) ambaye kwa sasa ataliongoza kwa muda baraza hilo akitangaza matokeo ya kura hizo alisema kura 20 zilikuwa zimemkataa Meya huyo kati ya kura 28 zilizopigwa.
Meya huyo anadaiwa kushindwa kufanya kazi yake na kusimamia kanuni na utaratibu za vikao vya halmashauri na kusababisha fujo bila kuchukua hatua kama kanuni zinavyomtaka.Kwamba katika vikao vyote alivyoendesha aliruhusu fujo kutokea na kusababisha aitwe kwenye kamati ya maadili ambayo aliidharau.
Kwamba alishindwa kutunza siri za halmashauri akiwa kiongozi mkuu wa madaiwani wa halmashauri ya Jiji la Mwanza,pia alishindwa kuzuia kuvuja kwa kabrasha la bajeti ya halmashauri hiyo,akishirki kikao kilichofanyika katika hoteli ya G&G Mei 13 mwaka huu.
Meya huyo tangu achaguliwe kiushika wadhifa huo alishindwa kabisa kusimamia mikutano ya Jiji, ikiwa ni pamoja na kusahindwa kusimamia ratiba za vikao na kanuni za halmashauri na kusababisha zogo la mara kwa mara kwa madiwani,ambao amekuwa akihoji maazimio ya mikutano anayoisimamia na kutia saini.
Ilidaiwa katika tuhuma hizo kuwa Manyerere akiwa Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza, alitia saini mikataba bila kupitishwa na vikao vya halali vya baraza la madiwani.anatuhumiwa kusaini mkataba wa Sheriff na kusababisha shule ya msingi Mbugani kuchukuliwa na taasisi ya watu binafsi kutoka serikalini.
Tuhuma nyingine ni kukataa kusaini mikataba halali iliyoazimiwa na baraza la madiwani, hivyo kuchelewesha utekelezaji wa miradi ya maendeleo ya Jiji la Mwanza, ambapo pia anatuhumiwa kutumia madaraka ya ofisi yake vibaya kwa kutoa upendeleo dhidi ya madiwani wenye uhusiano wa karibu naye ama wanaomwunga mkono.
Kabla ya Naibu Meya kutangaza matokeo hayo diwani wa Kata Sangabuye Bw.Dede Swila Dede alisimama na kuomba mwongozo ambapo alimtaka Meya Bw. Manyerere kupisha katika nafasi hiyo na kuchukuliwa na Naibu Meya Bw. Chichibela ili kuendesha kikao hicho na kutangaza matokea hayo.
“Tumepiga kura na madiwani waliosema kwamba Meya Bw.Manyerere ang’oke kwenye wadhifa huo ni wajumbe 20 na waliosema aendelee kubaki ni wajumbe nane tu (8 ) hivyo kwa mujibu wa matokeo hayo namuomba Mkurugenzi atusaidie kufafanua kanuni zetu zinasemaje”alisema Naibu huyo.
Madai ambayo yaliwasilishwa na madiwani hao kwa hoja iliyotolewa na Diwani wa CCM Kata ya Bugogwa, Dede Swila (CCM)na kuungwa mkonona Diwani wa Kata ya Igoma,Adam Chagulani (CHADEMA) wakati akichangia hoja kwenye baraza hilo kwa Diwani wa Kata ya Igoma (CHADEMA ) alionekana kuwahamasisha na kuwagusa baadhi ya wajumbe kwa kuiwasilisha upya baada ya Mkurugenzi kukataa barua ya hoja hiyo mwanzoni kwa madai kwamba haikufuata utaratibu na kanuni za vikao.
No comments:
Post a Comment