Thursday, September 6, 2012

KAJALA, MUMEWE HAWAIVI CHUNGU KIMOJA

Na Mwandishi Wetu
KUMBE mcheza filamu mkali Bongo, Kajala Masanja na mumewe, Faraji Augustine ambao wote wapo nyuma ya nondo katika Gereza la Segerea, Dar, hawaivi chungu kimoja.
Wawili hao wapo gerezani kufuatia kesi inayowakabili ya kughushi hati na kuuza nyumba iliyo kwenye pingamizi, wameonekana kutoiva kupitia salamu zao wanapokutana.
Mfano, ni kihoja kimoja kilichotokea hivi karibuni katika Mahakama ya Hakimu Mkazi,  Kisutu, Dar ambapo wanandoa hao walipelekwa kwa ajili ya kusilikilizwa kwa kesi hiyo.
Ni Kajala aliyeanza kuingia mahakamani hapo, moja kwa moja kwenye chumba cha hakimu halafu akafuatia mumewe na ndipo walipokutana macho na Kajala.
Huku wengi wakitarajia kuwasikia wawili hao wakisalimiana kwa kuchangamkiana, pengine na ‘kuhagi’ kiaina, hali ikawa tofauti. Hebu sikia hii.
Mume:  Hujambo?
Kajala: (huku uso wake ukionesha  kutoridhishwa na salamu hiyo na kukunja sura) Sijambo.
Kitendo hicho kiliwashangaza watu, licha ya kwamba ndugu wa karibu wa Kajala na Faraji hawakuonesha dalili za mshangao.
“Mh! Maskini, mume anajitahidi kumsalimia mkewe lakini mke anaonekana hapendi,” alisema mtu mmoja aliyekuwepo mahakamani hapo.
Awali  iliwahi kuripotiwa kwenye baadhi ya vyombo vya habari kuwa, Kajala anajuta kuolewa na mwanaume huyo kutokana na mkasa alioupata, kwamba anaamini umesababishwa na mumewe huyo na ndicho kitu  kinachomuuma staa huyo kila anapomuona mwanaume huyo.

No comments: