Thursday, September 6, 2012

NAY WA MITEGO AKOSA 'ADABU' UKWENI


SIKU chache baada ya mapenzi ya mkali wa michano ya Hip Hop Bongo, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ na mwigizaji Salma Jabu ‘Nisha’ kuvuja, mkali huyo wa muziki ameonekana kulikoroga ukweni kwake.
Kulikoroga kwa msanii huyo kulitokea siku ya ‘bethidei’ ya Nisha iliyofanyika Agosti 27, 2012 ambapo Nay alimtuma mdogo wake kwenda kumwakilisha huku akimwagiza amwambie mama wa Nisha kwamba yeye (Nay) ‘amekolea’ sana kwa binti yake na kweli mdogo mtu huyo akasema hivyo mbele ya waalikwa.
Kauli hiyo ilisababisha baadhi ya wageni hao kusema kuwa, Nay amefanya mambo ambayo kwa mila na utamaduni wa Kiafrika hayapo.
“Mtu huwezi kwenda kumwambia mama mkwe eti mimi nimempenda sana binti yako, lile ni tusi, alichotakiwa kufanya Nay ni kupeleka barua ya posa mambo yawe wazi,” alisema dada mmoja katika shughuli hiyo.

No comments: