Thursday, September 13, 2012

Magufuli kazini

Akagua Barabara Ya Kilwa

 Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli akijiridhisha kwa kupima kiwango cha lami inayowekwa upya katika barabara ya Kilwa na Kampuni ya Kajima ya Japan leo jijini Dar es salaam. Wengine wanaoshuhudia kutoka kulia ni mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Saidi Meck Sadiki, Balozi wa Japani nchini Tanzania Masaki Okada na baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya Kajima.
 Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli (mbele) akiwa amefuatana na balozi wa Japan nchini Tanzania Masaki Okada, Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam na viongozi wengine wa wizara akikagua moja ya sehemu ya barabara ya Kilwa inayojengwa upya na kampuni ya KAJIMA  ya Japan kutokana na barabara hiyo iliyokamilika hapo awali kuwa chini ya kiwango na serikali ya Tanzania kuikataa na kuiagiza kampuni hiyo iijenge upya kwa gharama zake.
  Wafanyakazi wakiendelea na ujenzi wa barabara ya Kilwa leo jijini Dar es salaam
 Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli akikagua ujenzi wa daraja la Kigamboni akiwa ameambatana na viongozi wa Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Saidi Mecki Sadiki (wa pili kutoka kulia) Mbunge wa Kigamboni Dkt.Faustine Ndugalile (wa tatu kutoka kulia) leo jijini Dar es salaam. Daraja la Kigamboni linajengwa na kampuni ya China Railways Engineering kwa gharama ya shilingi bilioni 214 na linatarajia kukamilika kabla ya mwaka 2015


 Mmoja wa wafanyakazi wa daraja hilo ambaye jina lake halikupatikana mara moja akiendelea na zoezi la kupiga picha huku akiwa amesimama kwenye mtando unaopitisha umeme mwingi bila kuchukua tahadhali wakati waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli alipokua akikagua maendeleo ya ujenzi wa  daraja hilo leo.
Picha na Aron Msigwa -MAELEZO

No comments: