Gari la kifaharia alilokuja nalo mutumiwa mahakamani
Kwa mara ya kwanza jeshi la Police Tanzania limetampeleka mtuhumiwa wa mauaji ya mwandishi wa habari Mwangosi kizimbani.
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi amesema askari
anayetuhumiwa kusababisha kifo cha aliyekuwa mwandishi wa habari wa kituo cha
televisheni cha Channel 10, marehemu Daudi Mwangosi amefikishwa mahakamani leo.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na wizara hiyo iliyosainiwa na Waziri Nchimbi
ilieleza kwamba Septemba 7,mwaka huu alikabidhiwa taarifa ya awali ya uchunguzi
wa polisi juu ya kifo cha mwandishi huyo na Mkuu wa Jeshi la Polisi, Inspekta
Jenerali Said Mwema.
Hivyo Septemba 11, mwaka huu aliliagiza Jeshi la Polisi kumpeleka mtuhumiwa huyo
askari namba G. 2573 PC Pasifious mahakamani leo kama ilivyotakiwa ma
Mkurugenzi wa Mshtaka(DPP).
Waziri Nchimbi alisema wakati mtuhumiwa huyo amefikishwa mahakamani , kamati
iliyoundwa chini ya Jaji Ihema itaendelea na kazi yake ili kupata suluhisho la
kudumu la migongano ya kikazi kati ya polisi na waandishi wa habari na waandishi wa
habari, polisi na vyama vya siasa ikiwemo kuboresha mahusiano zaidi kati ya polisi
na raia.
Aliongeza kuwa mkondo wa sheria umeanza kufuatwa nawaomba wadau wote kutoa nafasi
kwa utaratibu huo wa kisheria kufanya kazi.
Aidha aliongeza kuwa uchunguzi huo wa awali ulibaini mambo makubwa mawili ,ambayo
ni mlipuko uliotokea ulitokana na bomu la Machozi na bomu hilo lilifyatuliwa na
askari huyo.
No comments:
Post a Comment