litawahusisha wasanii mbali mbali wa hapa Tanzania.
Ujumbe maridhawa wa kinywaji maalumu cha tamasha la Fiesta.
Mdau akiwa amepozi ni fulana yake ya
fiesta mara baada ya kukabidhiwa na mwanadada Antu Mandoza ambaye ni
mmoja wa watangazaji wa Clouds TV,wakiwa ndani ya viwanja vya Biafra
mapema leo Kinondoni kwenye kuelekea kilele cha tamasha la Serengeti
Fiesta 2012.
" Hii ndio ya kwangu,ntaitinga kwa ajili ya kumuona Rozzzaaaay".!
" Daah hii inanitosha kabisa"!
Mtangazaji wa Clouds TV,Mussa Husein
akizungumza na mmoja wa mashabiki wa tamasha la Serengeti Fiesta
2012,ndani ya viwanja vya Biafra mapema leo jioni wakati skwadi zima la
lala salama kwenye kuelekea kilele cha tamasha la Serengeti Fiesta 2012
viwanjani hapo
Antu Mandoza akishoo love na baadhi ya mashabiki
Ni kushoo love tuu afuu Bhaaaaassss....!
Mussa Huseini pichani kati akiwa
amezungukwa na Mashabiki/wapenzi wa tamasha la Serengeti Fiesta wakiwa
wamejitokeza kwa wingi leo kwenye viwanja vya Biafra,wakati skwadi zima
la lala salama kwenye kuelekea kilele cha tamasha la Serengeti Fiesta
2012 lilipotinga kwenye viwanja hivyo na kutoa zawadi mbalimbali kwa
washabiki hao,ikiwemo fedha taslim,simu,tiketi za kuingilia kwenye
tamasha hilo pamoja na fulana.
Mashabiki na wapenzi wa tamasha la
Serengeti Fiesta wakiwa wamemzunguka kwa wingi mtangazaji Clouds FM,Dj
Fetty leo kwenye viwanja vya Biafra,wakati skwadi zima la lala salama
kwenye kuelekea kilele cha tamasha la Serengeti Fiesta 2012 lilipotinga
ndani ya viwanja hivyo na kutoa zawadi kem kem kem kwa washabiki
hao,ikiwemo fedha taslim,simu,tiketi za kuingilia kwenye tamasha hilo
pamoja na fulana.
Kama ada sehemu yenye mkusanyiko tunapeana riziki hivyo hivyo kwa namna moja ama nyingine masiha yanaendelea.
Mratibu wa kikosi cha lala salama
kuelekea kwenye kilele cha tamasha hilo hapo jumamosi,Mully B akitoa
maelekezo mafupi kwa baadhi ya watu waliojishindia tiketi za fiesta.
Mtangazaji wa Clouds FM,Dj Fetty
akifanya mazungumzo ya mmoja wa washindi aliyejishindia simu mapema
kwenye viwanja vya Biafra,Kinondoni jijini Dar.
No comments:
Post a Comment