Naibu
Waziri wa Ujenzi Mhe. Gerson Lwenge (katikati) akionyeshwa na Mtendaji
Mkuu wa TEMESA, Eng. Marcelin Magesa (kulia) maendeleo ya ujenzi wa
kivuko cha Msanga mkuu kama unavyoendelea kutekelezwa eneo la Kurasini
jijini Dar es Salaam. Kushoto mbele ni Eng. Rajab Ngome, Mkurugenzi
Msaidizi wa Ufundi kutoka Wizara ya Ujenzi.
Mhe.
Naibu Waziri wa Ujenzi Gerson Lwenge leo amefanya ziara ya kikazi
kutembelea Wakala wa Ufundi na Umeme TEMESA. Katika ziara hiyo Mhe.
Lwenge amewaasa wafanyakazi pamoja na Menejimenti ya TEMESA kufanya kazi
kwa weledi pamoja na moyo wa kutuma zaidi ili Wakala huo uweze
kufanikiwa katika majukumu yake.
Mhe.Naibu
Waziri ameitaka TEMESA kuangalia vyanzo vingine vya mapato, ikiwa ni
pamoja na kuongea na Taasisi za Fedha ambazo zinamasharti nafuu ya
mikopo ili kuongeza mtaji wake. Aidha, Naibu Waziri amehaidi kulivalia
njuga suala la madeni ambalo taasisi hiyo imekuwa ikizidai Wizara na
Idara mbali mbali za Serikali, hata ikibidi kuongea na Hazina ili fedha
za madeni hayo zikatwe moja kwa moja kutoka Hazina. Vile vile ameitaka
TEMESA kujenga hoja kwa vivuko ambavyo vinaendeshwa kwa hasara ili
Serikali iangalie gani inaweza kuwasidia hata kupitia kwenye Halmashauri
husika.
Aliongelea
usafiri wa boti kati ya Dar na Bagamoyo Mhe. Naibu Waziri ameiomba
TEMESA kuharakisha mchakato huo ili huduma hiyo iweze kuanza mara moja.
Awali
akimkaribisha Mhe. Naibu Waziri kuongea na Wafanyakazi, Mtendaji MKuu
wa Temesa Eng. Marcelin Magesa alizitaja changamoto mbali mbali
zinazokabili wakala huo ikiwa ni pamoja na kutolipwa madai yao kwa
wakati, kwa huduma zinazotolewa na TEMESA. Upungufu wa watumishi
kutokana na wengi kustaafu na wengine kufariki na kuwa mchakato wa
Serikali unachukua muda mrefu. Changamoto nyingine ni kuwepo kwa mapato
kidogo kwenye baadhi ya vivuko kiasi cha kutokidhi gharama za
uendeshaji. Mtendaji Mkuu huyo wa TEMESA ameiomba Serikali iangalie
uwezekano wa kuipatia taasisi hiyo mtaji ili imudu kukabiliana na
changamoto hizo pamoja na ubovu wa karakana na uhaba wa vitendea kazi
katika karakana zote nchini zinazo simamiwa na TEMESA
Wakati
huo huo akizungumzia suala la Dar – Bagamoyo ferry Mtendaji Mkuu
alisema tayari Wizara ya Ardhi imeshatoa Ramani kwa ajili ya maeneo ya
maegesho na tenda kwa ajili ya kumpata Mhandisi Mshauri zimefunguliwa
jana Jumatano tayari kwa kuanza kazi hiyo.
Taarifa Hii imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano kwa Umma
Wizara ya Ujenzi
No comments:
Post a Comment