Mkurugenzi wa Kampuni ya Linpo
Inmternational Agency,waandaaji wa Miss Tanzania, Hashim Lundenga,
akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Idara ya Habari
Maelezo jijini Dar es Salaam leo wakati wa kutangaza zawadi za Mshindi
wa Shindano la Redds Miss Tanzania 2012. Kulia ni Meneja wa Kinywaji cha
Redds, Victoria Kimaro.
Meneja wa Kinywaji cha Redds,
Victoria Kimaro akizungumza na Waandishi wa Habari katika Ukumbi wa
Idara ya Habari Maelezo jijini Dar es Salaam jana wakati wa kutangaza
zawadi ya Mshindi wa Taji la Reddds Miss Tanzania 2012. Kushoto ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Lino International
Agency,waandaaji wa Miss Tanzania, Hashim Lundenga. Kushoto ni Katibu
Mkuu wa Ka ya Miss Tanzania, Bosco Majaliwa "Mshua".
Kampuni
ya TBL kupitia kinywaji chake cha Redds Original ambao ndio Mdhamini mkuu wa
shindano la Redds Miss Tanzania 2012, leo tunatangaza zawadi kwa washiriki wote
wanaowania taji la Redds Miss Tanzania 2012.
Akizungumza
na waandishi wa Habari Jijini Dar Es Salaam Mkurugenzi wa kampuni ya LINO
AGENCY Hashim Lundenga alisema katika fainali za shindano la Redds Miss
Tanzania 2012 zitafanyika tarehe 3 Novemba 2012 katika ukumbi wa Blue Pearl
Hotel, (Ubungo Plaza) jijini Dar es
salaam ambapo ni shindano linaloshirikisha washiriki 30 kutoka mikoa mbalimbali
ya Tanzania.
Leo
hii tunapenda kuchukua nafasi hii kuwatangazia rasmi kuwa katika fainali ya
Redds Miss Tanzania mwaka zawadi zitakuwa kama ifuatavyo
Mshindi
wa Kwanza atapata zawadi ya pesa taslimu shs: 8,000,000/- pamoja na gari
Mshindi
wa pili atapata zawadi ya pesa taslimu shs: 6,200,000/-
Mshindi
wa tatu atapata zawadi ya pesa taslmu shs: 4,000,000/-
Mshindi
wa nne atapata zawadi ya pesa taslimu shs; 3,000,000/-
Mshindi
wa tano atapata zawadi ya pesa taslimu shs: 2,400,000/-
Mshindi
wa sita hadi wa 15 kila mmoja atapata shs: 1,200,000/-
Washiriki
wengine wote waliobaki kila mmoja atalipwa shs: 700,000/-
Katika
shindano hilo ambalo ndani yake kuna mashindano mengine madogo [Fast Tract]
tayari washiriki 3 wameshajipatia tiketi ya kuingia katika [Top 15 Finalist]
Washiriki
hao ni Lucy Stephano – Miss Photogenic
Magdalena Roy – Top Model
Mary Chizi – Top Sport Woman
Shindano
dogo lingine limepangwa kufanyika siku ya Ijumaa tarehe 26 Oktoba 2012 la
kumtafuta mrembo wenye Kipaji. Miss Talent.
Na
tarehe 28 Oktoba 2012 atapatikana Miss Personality.
Nae Meneja wa kinywaji cha Redds Original Bi Victoria
Kimaro amesema huu ni wakati sahihi wa kumpata mshindi biomba mwenye vigezo
sahihi hivyo kuwataka wapenzi wote wa tasnia ya urembo na wapenda maendeleo
kote nchini kujianda kupata tiketi za kushudia fainali hiyo mapema ili kuweza
kupata fursa ya kupata burudani mbalimbali.Kwa kweli shindano la mwaka huu
tunatarajia kuwa litafana sana hasa kwa kuzingatia kuwa maandalizi yote
yameshakamilika kwa kiwango kikubwa na sisi kama wadhamini wakuu tunahakikisha
kuwa mwaka huu kila atakaefika kwenye ukumbi wa Ubungo Plaza atakuwa na jambo
la kusimulia kwa sababu ni shindano la kipekee.
Baadhi ya warembo wanaowania taji hilo la Redds Miss Tanzania 2012 wakiwa ukumbini hapo wakisikiliza kutangazwa kwa zawadi yao.
No comments:
Post a Comment