UTETEZI TFF
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linapenda kuwataarifu kuwa Ofisa Habari wake, Boniface
Wambura ameteuliwa na SZhirikisho la Mpira wa Miguu la Afrika (CAF) kuwa mmoja wa maofisa
watakaoshughulikia masuala ya habari wakati wa fainali za Mataifa ya Afrika kwa Wanawake
zitakazofanyika nchini Equatorial Guinea.
Uteuzi huo umefanywa na Rais wa CAF, Issa Hayatou kwa ajili ya kufanikisha uendeshaji wa fainali hizo
za Mataifa ya Afrika kwa Wanawake zilizopangwa kuanza Oktoba 28, 2012 na kumalizika Novemba 11,
2012.
Wambura atakuwa mmoja wa maofisa watatu watakaoshughulikia habari kwenye fainali hizo. Wengine
ni ofisa kutoka makao makuu ya CAF, Mahmoud Garga na Arlindo Macedo kutoka Angola.
Wambura atakuwa ni Mtanzania pekee kwenye Kamati ya Maandalizi ya fainali hizo, kitu ambacho TFF
inajivunia kutoa mwakilishi kwenye moja ya mashindanoi makubwa ya mpira wa miguu Tanzania.
Rais wa TFF, Leodegar Tenga ameelezea uteuzi huyo kuwa ni matokeo ya kazi nzuri ambayo Wambura
amekuwa akiifanya tangu ajiunge na Shirikisho Januari mwaka 2011.
“Taarifa zake mbalimbali zimeifanya Tanzania iwe inang’ara CAF na hata FIFA kwa kuwa kwa sasa
wanajua kila kinachoendelea kwenye soka la Tanzania,” alisema Rais Tenga na kumtakia Wambura kila la
kheri kwenye kazi hiyo atakayoifanya kwa takriban siku 14.
Katibu Mkuu wa TFF, Angetile Osiah, akizungumza kwa niaba ya Sekretarieti, amemtakia Wambura kazi
njema na kwamba awe kioo cha mabadiliko makubwa yanayoendelea kwenye soka la Tanzania.
Wambura alijiunga na TFF Januari, 2011 akiwa mmoja wa waajiriwa watatu wapya kwenye Shirikisho
baada ya wsatendajiu wengine wawili kumaliza muda wao wa mikataba.
Wambura ni mwandishi wa habari mwandamizi ambaye ameshafanya kazi kwenye vyombo mbalimbali
kuanzia kazi ya uandishi hadi Mhariri Mtendaji wa gazeti la Jambo Leo ambalo alikuwa akifanya kazi
kabla ya kujiunga na TFF
Mahmoud Garga (CAF)
Boniface Wambura (Tanzania)
Arlindo Macedo (Angola
No comments:
Post a Comment