Friday, October 19, 2012

Tanzania Yaishauri ICC.

 Balozi wa  Ubalozi wa Kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Tuvako Manongi akizungumza wakati wa mjadala wa wazi ulioandaliwana Baraza Kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa na kufunguliwa na Katibu Mkuu Ban Ki Moon. Mjadala huo ulihusu uhusiano kati ya Amani na Haki na Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai ( ICC) miongoni mwa mambo aliyosisitiza Balozi Manongi ni pamoja na kuishauri ICC kutenda haki  bila kuegemea upande wowote na kwamba ijitahidi kujiepusha na ushawishi wa kisiasa kutoka  nchi yoyote ile likiwamo Baraza Kuu la Usalama.


Wajumbe wa Baraza Kuu la  Usalama la Umoja wa Mataifa katika mkutano wake wa wazi uliokuwa ukijadili uhusiano kati ya  Amani na Haki na Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai.
Na Maura Mwingira

No comments: