UMOJA
wa Mataifa (UN) umelaumiwa kwa kushindwa kuchukua hatua stahiki kuzuia
na kumaliza kabisa mgogoro unaoendelea katika mji wa Goma,Mashariki ya
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Shutuma hizo zimetolewa jana
jijini Dar es Salaam na Rais Yoweri Museveni, ambaye pia ni mwenyekiti
wa sekretarieti ya nchi za maziwa makuu,wakati wa mkutano wa Umoja wa
Jumuiya za Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) uliojikita
kuzungumzia migogoro ya Zimbabwe, Madagascar na Jamhuri ya Kidemokrasia
ya Congo.
Rais Museveni alisema kuwa kitendo
cha wanajeshi wa umoja wa mataifa wanaofikia 17,500 wa kulinda amani
DRC Kongo kuwepo huko bila kuwa na uwezo wa kukabiliana na waasi wa M23
wanaoendesha operesheni zao katika mji wa Goma ambao wameuteka mji huo
majuma mawili yaliyopita ni sawa na utalii wa kijeshi.
Akitoa historia ya mgogoro huo
Museveni alisema kuwa ulianza toka wakati wa Rais wa zamani wa nchi hiyo
wakati ikiitwa Zaire, hayati Mobutu Sseseko, na kueleza kuwa kwasasa
unaendeshwa na vikundi alivyoviita vya kigaidi.
Museveni alisema kuwa mgogoro huo
utaweza kutatuliwa kwa kutumwa kikosi cha pamoja cha nchi wananchama wa
SADC na nchi za maziwa makuu kitakachokuwa na amri ya kukabiliana na
uasi wowote katika eneo hilo.
Akifungua mkutano huo Rais Jakaya
kikwete,ameziomba nchi jumuiya za SADC kukomesha migogoro iliyozikumba
baadhi ya nchi hizo ili kuepusha maafa yanayoendelea kuwakumba wananchi.
Akizungumzia mgogoro wa Kongo,
kikwete alisema kuwa Tanzania itaendelea kushirikiana na nchi wanachama
wa SADC pamoja na nchi nyingine ili kuhakikisha amani ya kudumu
inapatikana nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
No comments:
Post a Comment