TARATIBU ZA KIMAHAKAMA ZAMKWAMISHA KURUDI NYUMBANI LEO!
Mahakama Kuu ya Tanzania mchana huu imeweka wazi masharti ya dhamana ya msanii wa filamu anayejulikana zaidi kwa jina la Lulu,. Lulu ambaye jina lake halisi ni Elizabeth Michael anakabiliwa na mashtaka ya kuua bila kukusudia ya msanii mwenzake(ambaye inasemekana walikuwa na mahusiano ya kimapenzi), Steven Charles Kanumba, kilichotokea April mwaka jana huko Sinza-Vatican jijini Dar-es-salaam.
Kwa mujibu wa chanzo chetu kilichokuwepo mahakamani mchana huu, dhamana ya mwigizaji Lulu ipo wazi endapo tu atatimiza masharti aliyotengewa ambayo ni
- Kuwasilisha au kukabidhi hati yake ya kusafiria(passport)
- Kutosafiri nje ya Dar es salaam.
- Kuripoti mahakamani kila siku ya kwanza ya kila mwezi
- Kuwa na wadhamini wawili ambao kila mmoja atamdhamini kwa shilingi milioni 20 za kitanzania.
Kwa maana hiyo, uwezekano ni wazi kabisa kwamba Lulu ataachiwa rasmi kesho January 29, 2013.
No comments:
Post a Comment