Monday, February 25, 2013

NAIBU WAZIRI WA FEDHA AKAGUA VITEGAUCHUMI VYA PSPF JIJINI DAR


SIKU MOJA baada ya Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF) kuwatembezea wadau na wanachama wake katika nyumba za mradi wa nyumba za makazi ambazo zimejengwa na Shirika hilo eneo la Buyuni kata ya Majohe Chanika Wilayani Ilala nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam,  Naibu Waziri wa Fedha, Janet Zebedayo Mbene nae ametembelea na kujionea nyumba hizo na kuumwagia sifa Mfuko huo kwa ubunifu na kuwajali wananchama wake.


Mbene pia alitembelea Ujenzi wa jingo la Kitegauchumi la Ghorofa 35 linalojengwa na Mfuko huo katikati ya jiji la Dar es Salaam.
Pichani ni Naibu Waziri wa Fedha, Janet Zebedayo Mbene akiangalia mchoro wa Jengo la Kitega Uchumi cha Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF) ambalo linajengwa katika ti ya jiji la Dar es Salaam na litakuwa na Ghorofa 35. Ndani ya jingo hilo la kutakuwa na Ofisi, maduka na nyumba za kulala.


Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF), Bwana Adam Mayingu akimpa maelezo Naibu Waziri wa Fedha, Janet Zebedayo Mbene juu ya muundo kamili wa Jengo hilo la ghorofa 35 ambalo linajengwa na PSPF jijini Dar es Salaam na litakuwa na maduka, makazi na Ofisi.

Meneja Mradi wa Ujenzi wa Jengo hilo la PSPF Tower, Ghazi Al Shamali (kushoto) akitoa maelezo kwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF), Bwana Adam Mayingu juu ya hatua zilizofikiwa hadi sasa katika ujenzi huo.
Naibu Waziri wa Fedha, Janet Zebedayo Mbene akiangalia thamani za ndani katika moja ya vyumba katika nyumba zilizopo ndani ya jengo hilo la PSPF Tower ambalo ujenzi wake bado unaendelea na pindi zitakapo kamilika zitauzwa  kwa watumishi wa Serikali pamoja na Wanachama wa Mfuko huo.

Naibu Waziri wa Fedha, Janet Zebedayo Mbene na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF), Bwana Adam Mayingu wakiongozana kuteremka ngazi zilizopo katika moja ya nyumba (apartment) zilizopo katika jingo hilo la PSPF Tower ambalo linaendelea kujengwa.


Naibu Waziri wa Fedha, Janet Zebedayo Mbene akitembezwa  ndani ya jengo hilo na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF), Bwana Adam Mayingu.

 Watumishi wa PSPF wakizungumza  jambo ndani ya Jengo hilo.

Awali Naibu Waziri wa Fedha, Janet Zebedayo Mbene alipata fursa ya kutembelea mradi wa ujenzi wa nyumba 491 za Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF) zinazojengwa Buyuni nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam na ambazo zimekamilika ujenzi wake na kuanza kuuzwa kwa Wanachama wa mfukjo huo. Pichani mbele kutoka kushoto ni Gabriel Silayo, Mkurugenzi wa Uwekezaji wa PSPF, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Adam Mayingu, Naibu Waziri wa Fedha, Janet Mbene na Mkurugenzi wa Fedha wa PSPF, Masha Mshomba wakimtembeza Kiongozi huyo katika nyumba hizo.


Nyumba hizo zikiwa zimekamilika ujenzi wake na kusubiri wateja tu.

Naibu Waziri wa Fedha, Janet Mbene akiwa na Mkurugenzi wa Fedha wa PSPF, Masha Mshomba akimtembeza ndani ya moja ya nyumba hizo.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Adam Mayingu akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Fedha, Janet Mbene nje ya moja ya nyumba ambazo zimejengwa na PSPF, kwaajili ya kuwauzia wanachama wake kwa gharama nafuu.

No comments: