MJANE ADHURUMIWA NYUMBA NA SERIKALI YA KIJIJI
Mjane Jerumana Nyinge 50 akiwa ndani ya kibanda chake alichotelekezwa na serikali ya kijiji
Hapo ndipo anapolala mjane huyo
Hivi ndiyo vyombo anavyotumia kupikia mjane huyo
Hiki ndicho kibanda alichopewa na serikali ya kijiji hii ni sura ya mbele ya kibanda hicho
Hii ni sura ya nyuma ya kibanda hicho
Humu ni ndani ya kibanda hicho kuna tundu kubwa kwenye paa la manyasi mvua ikinyesha mjane huyo hawezi kulala maana maji yote huingia ndani
Hakika mjane huyu anaitaji msaada angala nae apate bati choo godoro la kulalia na mahitaji mengine ya kibinadamu tunaomba tusaidiane kumsaidia mjane huyu
Mjane akiwa na jirani yake nnje ya kibada chake
Mwanamke aliyefahamika kwa jina la Jerumana Nyinge [50] mkazi wa kitongoji cha Usafwani kijiji cha Kongolo Mswiswi Kata ya Mswiswi wilaya ya Mbarali Mkoani Mbeya amedhurumiwa nyumba na serikali ya kijiji hicho.
Hii imekuja baada ya Mwanamke huyo kutelekezwa kwenye kibanda cha nyasi kwa zaidi ya miaka miwili sasa tangu nyumba yake ya bati ibomolewe ili kupisha shughuli za kimaendeleo kijijini hapo kwa ahadi kwamba angeweza kujengewa nyumba nyingine ya kuweza kuishi.
Mjane huyo ambaye hana watoto amejikuta akiishi kwa dhiki kwa kipindi chote cha masika ambapo baadhi ya vitu vimeharibika kwa kunyeshewa na mvua kikiwemo chakula pamoja na kukosa mahali pa kulala
“Mume wangu alifariki mwaka 2007 na kuanzia mwaka 2010 serikali ya kijiji imenihamisha na kunileta hapa bila huduma za msingi kama maliwato na bafu ambapo nimekuwa nikijisetiri kwa majirani na mara kadhaa wamekuwa wakinifukuza “ alisema mjane huyo.
Kwa upande wake jirani wa mjane huyo Bwana Mbwiga Mwayila amesema kuwa mjane huyo amekuwa akiishi maisha hatarishi kutokana na umbali mrefu anaotembea kufuata huduma ya maliwato na hasa nyakati za usiku amekuwa akiwagongea kuomba msaada huo na kuwa adha kwao kwa kuwakatisha usingizi .
Bi Salome Mwampashi ni jarani wa mjane huyo ambaye ameiomba serikali ya kijiji kumsaidia haraka mjane huyo ili kuepuka usumbufu kwa majirani huku akisema ameshuhudia mama huyo akipata taabu ya kupika wakati wa mvua kutokana na nyumba anayoishi kuvuja na moto kuzimika
Naye mwenyekiti wa kijiji hicho ambaye pia ni diwani wa Kata ya Mswiswi bwa Fulugence Mhegele amekiri kubomolewa kwa nyumba ya mjane huyo ilikupisha ujenzi wa maduka na kuleta maendeleo ya kijiji ambapo amefafanua hapakuwa na mapatano ya kulipa fidia ingawa diwani huyo hakuonesha mhutasari wowote wa makubaliano hayo .
Na Ezekiel Kamanga Mbarali
Kwa yeyote yule aliyeguswa kumsaidia mjane huyu
Piga simu namba hizi Ezekiel Kamanga 0754 49 07 52
Joseph Mwaisango 0754 37 44 08
No comments:
Post a Comment