Friday, March 22, 2013

INTERNATINAL FRIENDLY MATCH: BRAZIL 2 vs ITALY 2, MARIO BALOTELLI AISAWAZISHIA TIMU YAKE



International friendly, Stade de Geneve - Italy 2 (De Rossi 54, Balotelli 57) Brazil 2 (Fred 33, Oscar 42)

Huko Uswisi kwenye uwanja wa stade de Geneve, Brazil wakicheza na Italy, Timu zote zilianza kwa kushambulia na ha huku kila timu ikipania kumfunga mwenzake, mchezaji Fred wa Brazil ameanza kuifungulia timu yake bao katika dakika ya 33 kipindi cha kwanza baada ya ushirikiano mzuri kati ya Selecao na Filipe Luis kupigwa mpira wa juu kutokea upande wa pili kama kona na hatimaye Fred kuupata akiwa wa mwisho kuutokomezea nyvuni. Oscar dakika ya 42 akaipatia bao jingine la pili na kufanya 2-0. Mpaka dakika 45 zinaisha Brazil walikuwa wanaongoza kwa bao 2-0 dhidi ya Italy. LIVE: Italy 2-2 Brazil
Kipindi cha pili Italy walikuja kwa nguvu wakiwa nyuma ya bao 2 na dakika ya 54 mchezaji Daniele De Rossi akaipatia bao na kufanya 2-1 baada ya kazi nzuri ya Stephan El Shaarawy kupiga mpira huo.
Italy awakuishia hapo waliongeza bidii zaidi huku wakikosa mabao kadhaa na huku wakifanya mabadiliko. Dakika ya 57 baada ya dakika 3 kupita mchezaji mgeni na hatari wa AC Milan Mario Balotelli akaachia shuti kali la umbali wa yard 20 kutoka kwenye goli la Brazil na hatimaye kuishilia nyavuni huku kipa akibaki akiduwaa akipitwa na mpira huo kwa juu.

No comments: