Mkurugenzi Mtendaji wa Push
Observer, Rubelyn Alcantara akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo
katika hafla fupi iliyofanyika kwenye ofisini mwa Push Observer, Kinondoni.
Baadhi ya maofisa
kutoka makampuni mbali mbali wakielekezwa jinsi kampuni ya Push Observer
inavyofanya shughuli zake kutoka kwa mmoja wa wafanyakazi wa kampuni hiyo.
Na Mwandishi wetu
KAMPUNI za mitandao ya simu za
mikononi nchini zimeshika nafasi ya kwanza katika kutangaza biashara zao
kwenye vya habari nchini kwa robo ya mwisho ya mwaka jana.
Kwa mujibu wa takwimu
zilizotolewa na kampuni inayoongoza katika kusimamia na kufuatilia mwenendo wa
vyombo vya habari nchini, Push Observer, kampuni ya simu za mkononi ndio
zinaongoza katika orodha hiyo ya watangazaji bora pamoja na makampuni ya
vinywaji kwa kutangaza matangazo mengi nchini.
Mkurugenzi mtendaji wa Push
Observer, Ruby Alcantara alisema kuwa takwimu hizo ni za uhakika kutokana na
kukusanya rekodi hizo kwa kupitia vifaa vya kisasa walivyowekeza
katika sekta hiyo.
Alisema kuwa jumla ya fedha
zilizotumika kwa makampuni yote 20 bora katika kutangaza biashara ni sh
bilioni 17, 827,970, ingawa taarifa hiyo haija ainisha gharama halisi ya kila
kampuni ilizotumia katika kutangaza bidhaa zake.
“ Hatuwezi kuweka bayani ni
kiasi gani cha fedha kimetumika katika zoezi hili, ni vigumu kufanya hivyo,
lakini takwimu zetu ni sahihi kutokana na vifaa tulivyowekeza katika kutoa
huduma hii, ni ya kisasa na yenye ubora wa kimataifa, tutakuwa tunatoa taaifa
hizi kila baada ya miezi mine,” alisema.
Alisema kuwa vyombo vya habari
vinavyofaidika kwa kupata matangazo mengi ni redio na televisheni. Amesema kuwa
kampuni yao itakuwa inatoa taarifa kuhusiana na watangazaji bora wa kwenye
vyombo vya habari kila baada ya miezi mitatu. Ripoti robo ya kwanza ya
mwaka huu inatarajiwa kutolewa mwezi ujao mwanzoni.
“Ripoti hii inatoa fursa
kwa kila kampuni kujua utendaji wake katika ushindani wa kibiashara, pia kujua
mshindani wako anafanya nini katika kujitangaza na kukuwezesha kubadili
mbinu ili uweze kuendeleza ushindani au kuweza kuendelea kushika nafasi ya
kwanza kibiashara,” alisema.
No comments:
Post a Comment