Saturday, May 11, 2013

multchoice tanzania kusambaza digitali shule za msingi

ma f1130


Meneja Uhusiano wa MultiChoice Tanzania, Barbara Kambogi akiwakaribisha wageni wanahabari katika hafla mchapalo ya kusheherekea Africa Day na Dstv ambapo amesema DStv inatoa nafasi kwa wateja wake kuwa na fursa ya kuchagua vifurushi mbalimbali kulingana na uwezo wa mteja ambacho cha uwezo wa chini kabisa ni Access chenye zaidi ya channeli 40 gharama yake ni nafuu sana ambapo mteja atalipia shilingi 16,500 kwa mwezi.

Kwa kuendeleza hilo Multichoice ina mfumo wa kutoa elimu mashuleni ( Multichoice Resource Centre) hivyo watamumia jukwaa la Teknolojia kama darasa kwa njia mbalimbali kuwapa jamii nafasi ya kuendeleza vipaji na ujuzi.
Mfumo huo kutoa rasilimali kwenye shule kama vile ving’amuzi vya Satellite, VCRs/DVD na kifurushi cha elimu cha Dstv. Mpaka sasa Multichoice imeanzisha vituo vya rasilimali jamii katika shule 82 nchi nzima kwenye mikoa ya Arusha, Dar es Salaam, Dodoma, Iringa, Kagera, Mbeya, Pwani na Tanga.


ma1 a9e74
Meneja wa Fedha wa kampuni ya Multichoice Tanzania, Bw. Francis Senguji akizungumzia malengo ya DStv Tanzania ambapo amesema wao kama waendeshaji wa biashara nyingine barani Afrika wanaojali na kuthamini maendeleo ya jamii wameona ni wajibu kusaidia jamii ili kuweza kuendeleza maendeleo ya kijamii nchini Tanzania.

ma2 4d958
Meneja Uendeshaji wa Multichoice Tanzania, Ronald Shelukindo (katikati) akifafanua jambo wakati wa hafla mchapalo katika kusheherekea usiku wa Africa Day na DStv. Kulia ni Meneja Masoko wa Kampuni hiyo Furaha Samalu na kushoto ni Meneja Uhusiano wa Kampuni hiyo Barbara Kambogi.

ma3 7a261
Mkurugenzi wa Fullshangwe Blog John Bukuku akiserebuka na Meneja Uhusiano wa Multichoice Tanzania Barbara Kambogi wakati wa hafla hiyo.

No comments: