Jeshi la POLISI mkoani KAGERA limekamata jumla ya watuhumiwa
wa ujambazi SABA kati yao akiwemo mwanamke ambaye anadaiwa
kuwa ni kinara wa kupanga mipango
unyanganyi wa kutumia silaha na utekaji wa magari kwenye maeneo ya mapori
mbalimbali yaliyoko mkoani humo.
Akizungumza leo kaimu kamanda wa jeshi la POLISI mkoani
KAGERA, HENRY MWAIBAMBA ambaye ni
kamishina msaidizi jeshi hilo amemtaja kinara huyo wa ujambazi kwa jina la LEONCIA LOVATUS.
MWAIBAMBE amesema jeshi limefanikiwa kuwanasa watuhumiwa hao
kufuatia mpango wa muda mrefu wa jeshi hilo wa kufuatilia mtandao wa majambazi wanaojificha katika mapori kuteka magari na
kupora mali pamoja na fedha.
MWAIBAMBE amesema jeshi
hilo limefanikiwa kukamata BUNDUKI moja
aina ya SMG iliyokuwa inamilikiwa na watuhumiwa hao wa ujambazi, amesema
watuhumiwa hao wa UJAMBAZI walikuwa wameifadhi bunduki hiyo kwa mtu
mmoja aliyemtaja kwa jina la SABUHOLO
DAUD,ilikuwa na magazini moja na risasi KUMI NA SITA.
MWAIBAMBE amesema watuhumiwa walipoojiwa walikiri kutekeleza
matukioa makubwa ya uharifu ambayo ni pamoja na wizi wa utekaji wa magari na
wizi wa kutumia silaha.
Watuhumiwa walikamatwa ni pamoja na mwanamke kinara wa
kupanga mipango ya unyanganyi LEONCIA LOVAST ,SLAMBUKI ABEL, AMOS AMON, KABICHI
SYLIVESTER, HANANA FRANCIS, NDANDA ILIOFU na IMAN EZEKIEL.
No comments:
Post a Comment