Saturday, June 29, 2013

ARSENAL YAPAMBANA KUMSAJILI 'BRAZIL ONE', YATAKA DILI LIKAMILIKE HARAKA KUWAPIKU WAPINZANI


KLABU ya Arsenal itaangalia uwezekano wa kukamilisha usajili wa kipa namba wa Brazil na klabu ya Queens Park Rangers, Julio Cesar baada ya Kombe la Mabara.
Arsene Wenger anataka kipa mzoefu atengeneze ushindani kwa Lukasz Fabianski na Wojciech Szczesny.
Mazungumzo baina ya wawakilishi wa Cesar na viongozi wa Gunners tayari yamefanyika, lakini hayajamalizika kwa kuwa kipa huyo yupo kwenye majukumu ya kimataifa.
Wanted: Julio Cesar is set to join Arsenal following Queens Park Rangers' relegation to the Championship
Anayetakiwa: Julio Cesar anatarajiwa kujiunga na Arsenal kufuatia kushuka daraja kwa Queens Park Rangers
Wanted: Julio Cesar is set to join Arsenal following Queens Park Rangers' relegation to the Championship
The Gunners sasa inatarajiwa kumaliza dili hilo mara moja tu, baada ya kubainika Roma ya Italia nayo imeingia kwenye mbio za kuwania saini ya Cesar.
Kipa huyo wa kimataifa wa Brazil ambaye yupo huru kuondoka Loftus Road kufuatia kushuka kwa QPR hadi Championship, anataka kubaki London ambako amezoea maisha tangu awasili msimu uliopita akitokea Inter Milan.
Na The Gunners - ambayo inatumai kukamilisha pia usajili wa Gonzalo Higuain wiki ijayo, baada ya kocha wa Real Madrid, Carlo Ancelotti kufungua njia kwa mshambuliaji huyo kuondoka  Hispania - inajiamini dili hilo litakamilishwa baada ya Fainali ya Kombe la Mabara Jumapili.
Wenger alitaka kusajili kipa wa Stoke, Asmir Begovic na wa Liverpool, Pepe Reina lakini, licha ya kuwa na fungu la bajeti ya usajili la Pauni Milioni 70, kocha huyo wa Arsenal ameona  hana sababu ya kutumia fedha nyingi kwa ajili ya kipa.
Main man: Cesar impressed at Loftus Road despite the side's struggles in the Premier League
Mtu wa kwanza: Cesar amekuwa kivutio Loftus Road licha ya timu yake kuipa mkono wa kwaheri Ligi Kuu

Rangers itasikiliza ofa ya kiasi cha Pauni Milioni 2 kwa Cesar, wakati mshahara wake wa Pauni 70,000 kwa wiki halitakuwa tatizo kwa The Gunners, ambayo imetuma waangalia vipaji wake nchini Brazil kumuangalia Cesar anachokifanya katika Kombe la Mabara.
Pamoja na mpango wa kuwasajili Cesar na Higuain, The Gunners pia wanataka kumsajili beki wa Swansea, Ashley Williams na kiungo wa Everton, Marouane Fellaini. Lakini masuala ya kifedha yanatia saka kama Arsenal itaweza kusajili wachezaji wote hao.
Hadi sasa, Arsenal imegoma kumpa Fellaini mshahara wa Pauni 100,000 kwa wiki na pia imeshindwa kufika dau la Pauni Milioni 24 za kumnunua.
Missing out? Arsenal look set to be priced out of moves for Marouane Fellaini and Ashley Williams (below)
Amekosekana? Arsenal linataka kuwasajili Marouane Fellaini na Ashley Williams (chini)
Ashley Williams

No comments: