Warembo
12 wanaotarajiwa kupanda jukwaani Juni 15 mwaka huu kuchuana katika
shindano la kumsaka malkia wa urembo mkoani Kilimanjaro, Redds Miss
Kilimanjaro 2013 wameingia kambini leo.
Walimbwende
hao wanaotarajia kupambana kumpata Mrithi wa Redds Miss Kilimanjaro
2012, Anande Michael anayeshikilia taji hilo kwa sasa, wameweka kambi
katika hoteli ya Hugo, iliyoko nje kidogo ya mji wa Moshi.
Akizungumza
na Waandishi wa Habari, Mratibu wa Mashindano hayo, Mkurugenzi wa
Kampuni wa Rick Plan Company Ltd, Jackline Chuwa alisema ameamua
kuwaingiza warembo kambini mapema ili kuhakikisha kuwa mashindano ya
mwaka huu yanakuwa toofauti na ya mwaka jana.
"Warembo
wanaingia kambini Le, ili kuhakikisha kuwa mashindano yanakuwa ya
kipekee, tuimeboresha mamnbo mengio na lengo ni kumpata Redds Miss
Tanzania 2013, warembo wapo pale Hugo Hotel," alisema Chuwa.
Mkurugenzi
huyo alisema mashindano ya mwaka huu yatafanyika Juni 15 mwaka huu,
kuanzia saa moja kamili jioni katikia ukumbi wa La Liga Carnivore na
kuongeza kuwa viingilio ni sh. 15,000 kwa viti vya kawaida n ash. 30,000
kwa viti vya watu maalum (VIP).
Kuhusu
Burudani, Mkurugenzi huyo aliwataja wasanii wa Bongo Movie wakiongozwa
na JB, msanii wa kimataifa kutoka Burundi, Kidumu na Bendi yake, Ngoma
za asili na Sarakasi huku mgeni Rasmi akitarajiwa kuwa Waziri wa Mambo
ya Nje, Bernard Membe.
Redds
Miss Kilimanjaro 2013 inadhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL),
kupitia kinywaji cha Redds Original, Panone and Company Ltd, Bonite
Bottlers kupitia kinywaji baridi cha Cocacola na maji ya Kilimanjaro,
Mr. Price, Hugo Hotel na Kilimanjaro Express Bus.
REGARDS;
Fadhili Athumani
No comments:
Post a Comment