Watoto
wa Mkulima wakipeana ushauri...!!! Muasisi na Mwendeshaji wa Mtandao
huu wa Father Kidevu Blog, Mroki Mroki 'Father Kidevu' akimsikiliza kwa
makini Waziri Mkuu wa Tanzania, Mizengo Pinda (kulia) juu ya kilimo bora
cha umwagiliaji. Father Kidevu alitembelea Shambani kwa Waziri
Mkuukatika kijiji cha Zuzu kilichopo nje kidogo ya mji wa Dodoma
kujionea shughuli mbalimbali za kilimo ikiwepo ufugaji nyuki.
Waziri
Mkuu Pinda, alimwambia Father Kidevu kuwa kilimo chenye tija hakihitaji
eneo kubwa sana na pia Maji ni muhimu si kutegemea mvua ambazo hivi
sasa si za uhakika. "Ukiwa na Kisima cha maji katika shamba lako hapo ni
kila kitu, ardhi yeyote inaweza kubadilika"
Eneo
la shamba la Migomba iliyostawi vizuri la Waziri Mkuu. Pinda amewaasa
vijana kujiunga na kujikita katika kilimo kwani fursa hiyo ikitumiwa
vyema inaweza kumpa kipato mtu kuliko hata ajira ya maofisini.
Zabibu
zilizovunwa katika shamba la Waziri Mkuu Mizengo Pinda. Zabibu hizi
zipo za aina mbili za kutengenezea Mvinyo (Wine) na zile za Mezani
(Zabibu za kula kawaida). Father Kidevu Blog imebaini kuwa Asilimia
kubwa ya Zazibu zinazouzwa mitaani ni zabibu za kuzalishia Mvinyo
kutokana na naldha iliyopo katika Zabibu za kula.
No comments:
Post a Comment