Ijumaa Machi 30, 2012 | |||||||
Habari za Kitaifa Ngeleja awawakia waagizaji mafuta Imeandikwa na Mwandishi Wetu; Tarehe: 29th March 2012 @ 08:59 Imesomwa na watu: 201 |
|||||||
Badala yake, amesema yamekuwapo mafanikio mengi yakiwamo ya kupungua kwa msongamano wa meli bandarini; takwimu sahihi za ujazo wa mafuta yanayoingizwa nchini; ongezeko la kodi kwa Serikali; udhibiti wa upungufu wa mafuta yanayopotea wakati wa usafirishaji na kupungua kwa bei ya mafuta nchini. Akizungumza na gazeti hili ofisini kwake, Dar es Salaam jana, Ngeleja alisema wanaopinga mfumo wa uagizaji mafuta kwa pamoja ni wanyonyaji wa nchi na mawakala wa wanyonyaji, ambao wanafanya hivyo kwa maslahi binafsi. “Hawa ni wanyonyaji wa nchi na mawakala wa wanyonyaji ambao wanafanya hivyo kwa maslahi binafsi ili kunyonya Watanzania wenzao. Tunajua mfumo huo unapigwa vita sana na hili lilijitokeza kabla ya kuanza … lakini kwa ujumla, una faida nyingi na zimeanza kuonekana tangu uanze,” alisema Ngeleja. Akizungumzia dhana kwamba mfumo huo umesababisha hasara ya zaidi ya Sh bilioni 11 kutokana na hujuma katika ufunguaji wa zabuni ya pili Januari 27, alisema hilo si kweli na hakuna kampuni hata moja ambayo ingeokoa Sh bilioni 11. Alisema ufunguzi wa zabuni hufuata taratibu za wazi na kwa kuzingatia maelekezo yaliyomo kwenye hati za maombi, na kueleza kuwa Kampuni ya Addax ilikiuka maelekezo hayo ya hati za maombi, kwa kuwasilisha nakala tatu za maombi zikiwa kwenye bahasha moja wakati maelekezo ni kuwasilisha nakala tatu za zabuni (moja ikiwa katika nakala halisi, mbili zikiwa kwenye vivuli, zote katika bahasha moja yenye lakiri). “Wajumbe wote walikubaliana zabuni hiyo haikuwa halali na hivyo haikusomwa kama taratibu zinavyotakiwa. Kwa maana hiyo, mshindi alikuwa Augusta, Energy S.A. kwa wastani wa dola 67.50 za Marekani kwa tani. Mshindi wa pili alikuwa Reliance Industries Limited kwa wastani wa dola 70.83 kwa tani. “Kwa maana hii, nchi inatarajia kuokoa Sh bilioni 5.7 kama mafuta hayo yangeletwa na kampuni ya Reliance Industries Limited aliyekuwa na wastani wa dola 70.81 kwa tani. Aidha, kama Addax ingefuata taratibu za kuwasilisha zabuni, Taifa lingeokoa zaidi cha Sh bilioni 6.2. Hivyo basi taarifa hizo ni za uongo kuwa hakuna hata kampuni ingeokoa Sh bilioni 11,” alisema. Ngeleja alisema kama Kamati ya Kuratibu Mfumo wa Uagizaji Mafuta kwa Pamoja (PIC), ingepindisha sheria kwa kumpendelea Addax aliyekosea sheria za zabuni, mshindani yeyote angekwenda mahakamani, kusimamisha uagizaji mafuta hali ambayo ingeleta madhara makubwa. “Ewura imekuwa ikisisitiza kwa PIC kuwa ni muhimu kuzingatia matakwa ya sheria na kanuni katika uendeshaji wa shughuli zake hususan michakato ya zabuni. Uendeshaji wa zabuni kinyume cha matakwa ya sheria, kunaweza kusababisha malumbano ya mahakamani ambayo yataathiri upatikanaji wa mafuta nchini,” alisema Ngeleja na kutaja mafanikio ya mfumo huo. Alitaja pia kupungua kwa msongamano wa meli bandarini kutoka siku kati ya 40 na 60 zilizokuwa zinadaiwa na kampuni na hata siku 15 zilizoruhusiwa kwenye kanuni za ukokotoaji bei ya mafuta hadi kufikia wastani wa siku nne kutokana na utaratibu maalumu wa kuingiza meli bandarini. Alisema pia mfumo huo umeiwezesha Serikali kujua kiasi sahihi kinachoingizwa nchini na kinachotarajiwa kuingizwa nchini kwa siku za usoni, hivyo kupanga mipango sahihi ya kiuchumi kwa faida ya nchi kwa ujumla na kumekuwa na ongezeko la mafuta kwa asilimia 47 na hivyo pia kuongezeka kwa kodi. “Kumekuwa na udhibiti wa upungufu wa mafuta yanayopotea wakati yanasafirishwa kuja nchini. Hii inatokana na kwamba kwa sasa zinatumika takwimu halisi za mafuta yaliyopotea badala ya makadirio kwa utaratibu wa zamani,” alisema Ngeleja na kuongeza: “Mfumo huu umefanikisha kudhibiti ongezeko la bei kubwa zaidi ambalo lingekuwapo kama mafuta yasingeletwa kwa kupitia mfumo huu. Mathalani, gharama ya ucheleweshaji wa meli bandarini ni dola 30,000 kwa siku na mfumo huu umepunguza ucheleweshaji kutoka siku 15 hadi nne, hii imeingia kwenye gharama za mlaji. Bei zilizopo sasa zimedhibitiwa na mfumo huu.” Alieleza kuwa pamoja na malalamiko ya watu kwamba bei iko juu, kutokana na mfumo huu wa udhibiti wa bei wa Ewura, bado bei kwa Dar es Salaam ambapo mafuta hufikia, haijafikia bei iliyokuwapo miaka mitano iliyopita (2008) Sh 2,200 kwa lita kabla ya Ewura kuingilia kati. Hivi karibuni, ilidaiwa kuwa mfumo huo wa uagizaji mafuta kwa pamoja umeingia dosari baada ya kusababisha hasara ya Sh bilioni 11 kutokana na uzembe katika mpango mzima wa Machi – Aprili; hali iliyosababisha baadhi ya wafanyabiashara waagizaji wa mafuta kulalamikia uzembe huo kuwa unamwumiza mtumiaji wa mwisho na kumpatia faida maradufu mwagizaji. |
FOUR WAYS INTERNET & STATIONERY WANASHUGHULIKA NA USAMBAZAJI WA VIFAA VYA SHULE NA MAHITAJI MENGINE YA MAOFISINI IKIWA NI PAMOJA NA HUDUMA YA INTERNET MASAA 17 KWA SIKU INAFUNGULIWA SAA 7:00 HADI SAA 10:00 USIKU K A R I B U S A N A
Wednesday, March 28, 2012
News
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment