MAHAKAMA
ya wilaya ya Bukoba imemhukumu Mathayo Bagaichwaki (40) mkazi wa mtaa
wa Nyamkazi ulioko katika manispaa ya Bukoba kwenda jela miaka kutumikia
kifungo cha miaka 30 baada kupatikana na kosa la kumbaka binti mwenye
umri wa miaka 15.
Hukumu
hiyo ilitolewa jana na hakimu mfawidhi wa mahakama ya Bukoba, Charles
Uisso baada ya kuridhika na ushahidi uliotolewa katika mahakama hiyo na
mashahidi upande wa mashitaka uliiongozwa na wakili wa serikali Chema
Mbena.
Pia
hakimu huyo aliridhika na ushahidi ulitolewa na binti aliyefanyiwa
unyama huo baada ya kuielezea mahakama jinsi alivyobakwa na Bagaichwaki
kabla ya kuokolewa na wazazi wake walioshirikiana na majirani.
Katika
hukumu hiyo mahakama hiyo haikuridhika na ombi la utetezi lililokuwa
limetolewa na Baigaichwaki aliyedai mashtaka yaliyokuwa yanamkabili ya
ubakaji kuwa yalikuwa yakubambikizwa.
Alikuwa
ameielezea mahakama kuwa alibambikizwa kesi hiyo kwa kuwa alikuwa
akimdai baba mzazi wa binti aliyembaka kiasi cha shilingi 50,000.
Wakati
wa hukumu hiyo ikitolewa mwendesha mashtaka wa serikali aliielezea
mahakama kuwa mstakiwa hakuwa kumbukumbu zozote za uharifu ila aliiomba
mahakama itoe adhabu kali kwa mstakiwa.
Alisema
adhabu kali ikitolewa dhidi ya mshtakiwa itakuwa fundisho kwa watu
wazima wenye tabia ya kujihusisha na vitendo vya ubakaji hasa kwa watoto
wenye umri mdogo.
Awali
mwendesha mashtaka aliielezea mahakama kuwa April 18,mwaka huu,
Gabaichwaki katik maeneo ya nyamkazi alimbaka msichana mwenye umri wa
miaka 15 nyumbani kwake.
No comments:
Post a Comment