Dar es Salaam.Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za
Serikali(CAG) ameanza ukaguzi maalumu katika Halmashauri ya Bukoba Mjini
kuhusu ubadhirifu wa fedha mbalimbali za miradi ya maendeleo zilizokuwa
zinatumika kwenye halmashauri hiyo.
Uamuzi wa CAG umekuja baada ya Kamati Kuu ya CCM
kumtaka CAG kufanya ukaguzi katika halmashauri hiyo baada ya kuwepo kwa
taarifa za ubadhirifu wa fedha za miradi ya maendeleo zinazodaiwa
kuidhinishwa na Meya wa Halmashauri hiyo, Anatory Aman.
Miradi hiyo ni pamoja na mradi wa upimaji wa
viwanja vya Mji wa Bukoba, ukarabati wa soko na ujenzi wa stendi kuu ya
mabasi ambayo inadaiwa kuwa na harufu ya ufisadi.
Akizungumza na gazeti hili Dar es Salaam jana,
Msaidizi wa CAG, Fransic Mwakapalila alisema ukaguzi huo utaanza mwezi
huu, ambao utahusisha kukagua miradi mbalimbali iliyoainishwa kwenye
hadidu za rejea.
Alisema kutokana na hali hiyo, wakaguzi watafika kwenye halmashauri hiyo mwisho wa mwezi huu kwa ajili ya kufanya ukaguzi huo.
“Tayari tumepewa hadidu za rejea kwa ajili ya
kufanya ukaguzi maalumu wa Halmashauri ya Bukoba mjini, hivyo basi
wakaguzi watafika katika halmashauri hiyo mwisho wa mwezi huu,” alisema
Mwakapalila.
Aliongeza kuwa kutokana na hali hiyo, muda wa
kukamilika kwa ukaguzi huo utatokana na kukamilisha kwa shughuli hiyo,
jambo ambalo linaweza kubaini ukweli kuhusu uhalali wa matumizi ya fedha
hizo au la.

No comments:
Post a Comment