Thursday, August 21, 2014

Marekani yaishambulia IS licha ya onyo


Bwawa la Mosul lililotekwa kutoka kwa wapiganaji wa IS
Majeshi ya Marekani yameendelea kuwashambulia wapiganaji wa Islamic State huko Iraq licha ya vitisho kutoka kwa kundi hilo kuwa watawaua mateka wengine wamarekani iwapo Obama angeendelea kuishambulia himaya hiyo kaskazini mwa Iraq.
Majeshi ya Marekani kwa ushirikiano na ndege zisizikuwa na marubani zilifanya mashambulizi 14 usiku wa kuamkia leo.
Mashambulizi kumi na manne ya angani yamefanyika katika eneo karibu na bwawa la Mosul na yalilenga kuwasaidia wanajeshi wa Iraq na wa kikurdi.

Bwawa la Mosul lililotekwa kutoka kwa wapiganaji wa IS
Maafisa wajeshi la Marekani wamesema kuwa walifaulu kulipua magari ya kijeshi na vitu vingine vilivyokuwa vikitumiwa na wapiganaji wa IS .
Tarifa kutoka kwa wakurdi zinasema kuwa ndege ambazo hazina rubani zilikuwa angani kuwalinda wanajeshi Wakurdi wakati wapiganaji wa Pesh Merga wakisukumwa katika milima, kusini mashariki mwa bwawa kubwa la Mosul, ambalo lilitwaliwa tena kutoka kwa wapiganaji wa kiislamu wiki hii.
Pentagon imethibitisha kuwa mashambulizi kumi na manne ya angani yalifanywa katika sehemu hiyo kuliko bwawa na kuyalenga magari kadhaa ya kijeshi na vitu vingine.
Televisheni ya taifa ya Iraq imesema kuwa ndege hizo za vita za Marekani zilikuwa pia zimetekeleza mashambulizi katika kambi za magaidi mkoani al-Anbar hadi magharibi mwa Baghdad, na zilikuwa zimetoa ulinzi wa angani kwa vikosi vya serikali vilivyokuwa vikielekea kuwakabili waasi wa kisuni.

Majeshi ya Iraq yakielekea kukabiliana na wanamgambo wa Islamic State
Awali makao kuu ya Jeshi la Marekani limesema kuwa wanajeshi la kitengo maalum walijaribu kumuokoa mwanahabari James Foley na waamerika wengine walioshikwa mateka nchini Syria.
Habari hii imetolewa baada ya video ya aliyetekwa nyara novemba 2012 nchini Syria kuonyeshwa akiuawa kikatili na wanamgambo wa Kiislamu kutokea jumapili .
Wanamgambo hao walisema mauaji yake ilikuwa kulipiza kisasi dhidi ya Marekani kwa sababu ya kuwashambulia wapiganaji wao hewani Iraq.

Mwandishi aliyeuawa na kundi la IS
Rais wa Marekani Barack Obama alikashifu mauaji hayo na kuwalinganisha wanamgambo hao na ugonjwa wa saratani na kuwa itikadi zao hazikuwa na mwelekeo aliendelea kuwa kusema tendo hilo lilishtua ulimwengu mzima

Umoja wa kitaifa ,uingereza na wengine pia wameeleza huzuni yao kutokana na video hiyo.
Mamake Bwana Foley Diane alisema kuwa mwanawe aliaga dunia kwa niaba ya watu wa Syria.
Kamati inayolinda wanahabari ilisema ina wasi wasi kwa wanahabari wote waliozuiliwa na wanamgambo hawa na kusema wanahabari wajiepushe na Syria.

No comments: