Ni mgomba aina ya mtishwe ambalo ndilo tumaini la mwanabukoba kutokana na migomba ya asili kushambuliwa na wadudu (mnyauko)
Nikiongea na bwana shamba katika ofisi yake jina limeifadhiwa amesema kuwa mpaka sasa hamna ufumbuzi uliokwisha tangazwa juu ya ugonjwa wa mnyauko unaoshambulia migomba ya asili. Labda jambo ambalo mpaka sasa tunalifanya ni kumshauri mkulima anapoona dalili za ugonjwa huo kwenye shamba lake afanye kila liwezekanalo kung`oa mgomba huo na kuufukia mara moja kwani inasemekana ugonjwa huo unasambaa kwa njia ya hewa.
Ni katika soko kuu la Manispaa ya Bukoba hapa nikiongea na wadau wa ndizi za asili wanasema hali ni mbaya sana kwani kila muuza ndizi za asili ndani ya soko hilo anasema kuwa ndizi zimeadimika. Mapaka sasa wilaya zinazoweza kutoa ndizi za asili kwa wingi ndani ya mkoa wa kagera ni Wilaya ya Karagwe ikisaidiana na Wilaya ya Mleba.Je bei ya ndizi hizo ni shilingi ngapi "kaka siwezi kusema kuwa kuna ndizi ina bei alisi bali kila mtua anauza kadili anavyojifikia ili kuweza kupata faida na kurudisha mtaji wake ila bei ya chini ni shilingi 13000 na kupanda hadi shilingi 30000 kwa ndizi moja "
BUKOBA BILA NDIZI INAWEZEKANA ?
Unaweza toa maoni yako kupitia kwenye sehemu ya maoni au kwa kupiga simu ya kiganjai 0768078360
OFISI YA AIR PORT BUKOBA
Sasa uaneza kunda Mwanza na Kurudi kwa Bei nafuu pia kuna usafili wa kukodi mda wote.
No comments:
Post a Comment