Sunday, March 25, 2012

 

Ni manufaa gani yatapatikana kwa Tanzania kujiunga na Mpango wa kuendesha shughuli za Serikali kwa Uwazi (OGP)? Wabunge Zitto Kabwe na January Makamba ni sehemu ya wachangiaji wa maoni hayo.

AJARI MBAYA YA MOTO YATOKEA KWA BASI LA  SUPER NAJMUNISA LIKIWA KATIKA SAFARI ZAKE MKOANI MOROGORO.

Basi la Abiria la kampuni ya Super Najmunisa lifanyalo safari zake kati ya Dar es Salaam na Mwanza. likimalizikia kuteketea kwa moto mara baada ya kupata shoti ya betri.ajali hiyo imetokea jioni ya jana maeneo ya Berege Mkoani Morogoro wakati basi hilo likiwa njiani kuelekea jijini Dar es Salaam kutokea Mwanza. hakuna mtu yeyote aliedhulika kwenye ajali hiyo isipokuwa mizigo yote ya abiria hao iliteketea kwa moto.
Basi hilo nikiendelea kuwaka moto.
Sehemu ya Abiria wa Basi hilo pamoja na wamazi wa maeneo ya jirani na kijiji hicho wakiwa wamekaa pembeni kuangalia jinsi gari hilo linavyoteketea kwa moto bila ya wao kujua la kufanya wakati huo.

UWOYA adhalilika

IKIWA ni siku chache tangu mumewe, Hamad Ndikumana ‘Kataut’ alipoondoka Bongo, Irene Pancras Uwoya anadaiwa kudhalilika ukumbini baada ya kigauni kifupi alichotinga kushindwa kumsitiri hivyo ‘kufuli’ lake kuwa nje nje, aya zifuatazo zina undani kamili.
Tukio hilo la kusikitisha lilichukua nafasi ndani ya Ukumbi wa Business Park Kijitonyama, Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki iliyopita ambapo kulikuwa na ‘bethidei’ ya mwaka mmoja ya Klabu ya Bongo Movie.

MAPEDESHEE WAJIPITISHA
‘Shushushu’ wa gazeti hili aliwashuhudia wanaume hasa mapedeshee wakijipitisha mbele ya meza aliyokuwa amekaa Uwoya na mwigizaji mwenzake, Blandina Chagula ‘Johari’.
Hata hivyo, ilielezwa kuwa kilichomponza Uwoya ni kigauni alichovaa kifupi kilichosababisha nguo hiyo ya ndani nyeupe kuonekana kirahisi alipokuwa amekaa.
NENO LA WADAU
“Duh! Mama Krish (Uwoya) katoka bomba lakini kile kigauni kinamdhalilisha, kinaonesha kufuli yake nyeupe.
Ukweli ni kwamba angekuwepo Ndiku (mumewe) asingefanya hivyo kwa sababu angemlindia heshima,” alisema mmoja wa wadau  waliomshuhudia staa huyo ambaye muda mwingi alikuwa kimya ukumbini humo.
UWOYA VIPI?
Jitihada za kuzungumza na Uwoya juu ya tukio hilo hazikuzaa matunda kufuatia simu yake kuita bila kupokelewa.
Hivi karibuni Ndiku alitimka Bongo na kwenda kwao Rwanda kujiunga na timu ya Rayon Sports huku akimwacha mkewe huyo na mwanaye Krish.  

Rais Kikwete awaapisha Makatikbu Tawala wa Mikoa ikulu jijini Dar Es Salaam


Katibu Tawala mpya wa mkoa wa Mbeya Bibi.Mariam Mtunguja akila kiapo mbele ya Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete ikulu jijini Dar es salaam leo.Katika hafla hiyo Rais aliwaapisha pia makatibu Tawala wa mikoa mingine kama ifuatavyo,Dkt. Faisal Issa (Kilimanjaro),Bwana Eliya Ntandu (Morogoro), Bwana Severine Kahitwa (Geita),Bwana Emmanuel Kalobelo (Katavi), Bwana Hassan Bendeyeko (Ruvuma) na Dkt. Anselem Tarimo (Shinyanga). 

Bonanza la Waandishi wa Habari (Media Day) lafana sana leo jijini Dar

Beki wa timu ya Dira, Makubuli Ally (kushoto) akijaribu kuwazuia wachezaji wa IPP, wakati wa Bonanza la waandishi wa habari (Media Day) lililofanyika Msasani Beach jijini Dar es Salaam leo. Bonanza hilo limeandaliwa na TASWA na kudhaminiwa na TBL. Dira ilishinda 3-1.

Mchezaji wa Kick Boxing wa timu ya Free Media, Agness Yamo, akipambana na mchezaji wa TSN, Adam Amon wakati wa Bonanza la waandishi wa habari (Media Day) lililofanyika Msasani Beach jijini Dar es Salaam leo, na kudhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL). Agnes Yamo alishinda kwa Pointi.



Waandishi wa Habari toka vyombo mbali mbali nchini wakiwa kwenye Bonanza hilo la waandishi wa habari (Media Day) lililofanyika Msasani Beach jijini Dar es Salaam leo, na kudhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL).


No comments: