Wasamaria Wema: Gomery anahitaji Msaada wa Usafiri hasa Bajaj
Gomery Kotey ni mkazi wa Gairo mkoani Morogoro ambako alizaliwa mwaka 1970.
Huyu bwana amekuwa na matatizo ya kiafya kwenye mifupa kwani amekuwa anavunjika mara kwa mara hali ambayo imemfanya ashindwe kutoka eneo moja kwenda jingine.
Historia ya maisha yake kwa mujibu wa dada yake Bi. Olivia Kotey ni kwamba mdogo wake huyu alizaliwa na kichwa kikubwa na mwili mwembamba lakini alipatiwa matibabu katika hospitali mbalimbali na kupona tatizo hilo.
Hata hivyo baada ya hapo Gomery alipata tatizo jingine la kuvunjika mifupa ambapo liliendelea hadi kuwa ni kubwa kwani alishavunjika miguu yote miwili mara tatu na mikono yote miwili mara mbili hali inayompelekea kushindwa kutekeleza majukumu yake yanayompatia riziki ya kila siku.
Aidha alishavunjika taya hali iliyofanya kupoteza meno ya taya la chini. Kwa upande wa tiba madaktari wanasema kuwa huo ulemavu wa kuzaliwa.
Kutokana na hali hiyo Kotey chombo kinachoweza kumsaidia kutembea au kutoka eneo moja hadi jingine ni Bajaj. Hiyo inatokana na sababu kuwa vyombo vingine visivyo vya moto kama baiskeli hataweza kuitimia kutokana na uimara wa mifupa yake kuwa ni mdogo.
Kwa yeyote anayeguswa na kuwa na moyo wa kutoa awasiliane na wafuatao; +255718659413/+255712155221/

No comments:
Post a Comment